Thursday, September 6, 2012

Habari njema kwa Wazanzibari....


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China leo zimetiliana saini Mkataba juu ya Mashirikiano ya Kiuchumi na Kiufundi ambapo Zanzibar itapatiwa jumla ya RMB 60 Millioni sawa na TZS,14.8 BILLIONI.

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi Fedha ,Uchumi na Mipango ya Maendelro Omar Yussuf Mzee ndie alietia saini na kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Naibu Waziri wa Biashara Zhong Shan ndie alietiana saini ambapo ulishuhudiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali Idd na kwa upande wa China Naibu Waziri Mkuu wa nchi Hui Liangyu.

Kwa mujibu wa Mkataba huo wa Mashirikiano Zanzibar itafaidika katika Ujenzi wa Majengo mapya na Ukarabati mkubwa wa Majengo yaliopo katika Hospitali ya Abdulla Mzee ..Pia Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Mwananakwerekwe.Halkadhalika Zanzibar itafaidika katika utiaji wa Taa za Barabarani zitakazotumia Nishati ya jua katika baadhi ya Barabara kuu za Mjini.

Aidha Mkataba huo unaelezea kuwa Zanzibar itapata Mafunzo Mafupi na Marefu katika Fani tofauti ambayo itapendekezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Mbali na hayo pia kutakuwapo Uchimbaji wa Visima vya Maji pamoja na maeneo mengine ambayo Nchi mbili zitakubaliana.

Pia ujumbe huo wa China umetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya msaada wa Wataalamu wanne(4) kutoka China ambao watakuwepo Zanzibar kwa miaka miwili(2) ambao watawafundisha Mafundi wa Mitambo wa Studio yakurushia matangazo ya Redio pamoja na kutoa Vifaa mbali mbali kwa ajili ya Studio hiyo.

Ujumbe huo wa China ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu uliwasili Zanzibar leo jioni na kupokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwamo Mawaziri. Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu pamoja na maofisa mbali mbali wa Serikali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein jioni hiyo hiyo alikuwa na Mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu Ikulu ambapo walizungumzia juu ya Ushirikiano kati ya Nchi zao.

Usiku huu Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Amemuandalia Chakula Naibu Waziri Mkuu wa China pamoja na ujumbe wake huko katika hoteli ya Lagemma Nungwi.

Kesho asubuhi Naibu Waziri Mkuu wa China na ujumbe wake watatembelea kanisa la Anglican Mkunazini na baadae kuelekea Beit el Ajaib na Jumba la Wananachi Forodhani na kuelekea Uwanja wa ndege kwa kurejea Dar es Slaam.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
6/9/2012

No comments:

Post a Comment