Sunday, September 2, 2012

Wabunge wa bunge la jumuiya ya Afrika mashariki wawaahidi mambo mazuri watanzania katika vikao vitakavyoanza kesho jijini Nairobi.

 Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika bunge la jumuiya ya Afrika mashariki Adam Kimbisa akisisitiza jambo katika mkutano huo leo.


Katibu  wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji, akisisitiza jambo katika mkutano huo.





Wabunge wa bunge la Afrika ya Mashariki upande wa Tanzania wameapa kuulinda mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki kwa kuufanyia kazi katika kikao cha  Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya.

Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha kwa waandishi na watanzania kwa ujumla.

Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatarajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya.

Aidha wabunge hao sita pia walizungumzia tofauti za kiuchumi katika nchi hizi tano zinazounda jumuiya hiyo na kusema kuwa watanzania hawapaswi kukata tamaa na badala yake wafanye kazi kwa juhudi na kuzitumia fursa za jumuiya hiyo ili kuweza kuwa mbele katika uchumi na maendeleo.

Picha zote kwa hisani ya MAELEZO. 

No comments:

Post a Comment