Wednesday, October 3, 2012

Ilala ina-Take off...........

 Meya wa Ilala kijana Jerry Silaa, akionyesha namna ya ukusanyaji kodi chati inavyopanda juu zaidi.

 Mstahiki meya wa wilaya ya Ilala, Jerry Silaa akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Arnaoutoglu mnazi mmoja kuhusu mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Ilala na na hali halisi ilivyo katika bajeti ya 2012-13. Pembeni yake ni naibu wake ndugu kessy.


Na: Honest Arroyal

Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, kupitia meya wake, Mhe. Jerry Silaa jumatatu ya Oktoba 1, 2012 limekutana na waandishi wa habari pamoja na wafanyabiashara katika ukumbi wa Arnaoutoglo kuzungumzia kwa ufupi juu ya utendaji wa shughuli za manispaa ya ilala kwa mwaka wa fedha 2011/2012

Manispaa ya Ilala kwa mwaka uliopita imefanya jitahada kubwa juu ya ukusanyaji wa mapato huku ikipitia changamoto mbalimbali ambazo baadhi zimepatiwa ufumbuzi.

Kwa ujumla, ukusanyaji wa mapato ulikusudiwa umepanda kutoka 88% kwa mwaka wa fedha 2010/2011 mpaka Shilingi 17.1 bilioni zilizokusanywa mwaka huu kiasi ambacho ni sawa na 99% ya mafanikio ya malengo. Ongezeko hilo limetokana na kugundua vyanzo vingi vya mapato kwa 102% ambavyo ni Shilingi 2.25 bilioni kutoka katika mabango ya matangazo yaliyopo barabarani. Kiwango hicho kimeongezeka kutoka shilingi 1.47 bilioni ya mwaka jana mpaka shilini 2.25 bilioni mwka huu. 

“Leo tumewalika walipa kodi wakubwa katika manispaa ya Ilala ambao mchango wao katika uchumi wetu umekuwa mkubwa sana. Sababu kubwa ikiwa ni kuwapa walipa kodi taarifa fupi na kuwashukuru kwa mchango wao katika maendeleo ya manispaa yetu. ”Alisema Silaa.

Kitengo kingine kilichoonyesha mafanikio ni kile kinachotoa leseni za ujenzi ambacho kimechangia ongezeko la 205% ambalo ni shilingi 307 milioni kutoka shilingi 154 milioni ya mwaka wa jana. 

Kutoka shilingi 2.14 bilioni za makusanyo ya mapato kutoka kwenye kodi ya thamani, lengo hili lilishuka kwa kiasi kikubwa mpaka 54% kutoka kwa malengo yaliyowekwa ukilinganisha na 74% kwa mwaka jana. Sehemu iliyofanya vibaya kabisa kwa mwaka huu katika ukusanyaji wa mapato ni mapato kutoka leseni za biashara ambayo 0%.

Kutokana na kutofikia malengo, kazi za maendeleo zilizopangwa na halmashauri kwa ajili ya maendeleo zimekuwa na changamoto kubwa. Mwaka wa fedha wa 2012/13 umeshapangwa na tunatarajia kuomba msaada si tu kwa Wafanyabiashara na wakazi wa Halmashauri wa manispaa ya Ilala kwa kiasi kikubwa ila pia tunaitegemea serikali kuu katika hili. Asilimia 49 tu ya bajeti ndiyo imepatikana tayari kwa mataumizi ya miradi ya maendeleo ya manispaa.

 “Manispaa ya Ilala ipo katika moyo wa jiji la Dar es salaam, na nchi kwa ujumla kutokana na ofisi nyingi za serikali, ofisi nyingi za makampuni pamoja na ofisi za kibalozi zipo katika Halmashauri yetu, kutokana na hilo, ninaomba Serikali kuangalia juu ya ufanikishaji wa mapendekezo wa bajeti yetu kwa mwaka wa fedha 2012/13 kwa asilimia 100 ili kuweza kufanikisha mahitaji muhimu ya maendeleo ya Halmashauri na kuwezesha ufanyaji wa shughuli mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri yetu” alisisitiza Silaa.  




No comments:

Post a Comment