Friday, October 12, 2012

Leo Maeneo ya Mbagala Chamazi kulikuwa na vurugu nyingi sana kufuatia Mtoto wa kidato cha kwanza kukinajisi kitabu Kitakatifu cha Qur an. Waislamu wa Dar es Salaam kabla na baada ya sala ya Ijumaa walitaka kumchinja mtoto huyo lakini Polisi waliwazuia. Kwa hasira waislamu wakaanza kuchoma makanisa na kudhihirisha hasira yao kwa kupambana na jeshi la polisi.

 Jeshi la polisi kitengo cha kutuliza ghasia wakijiandaa kuwazuia Waislamu wenye hasira kali huko Mbagala.


 Huyu kijana inadaiwa alipigwa kupita kiasi hivyo jeshi la polisi liliamua kumtelekeza ili asiwafie mikononi.



 Hapa wanahabari wakiangalia moja ya makanisa matatu yaliyochomwa na kuharibiwa vibaya kufuatia vurugu hiyo.




                                                                        Balaa linaendelea.





 Hili ni gari la Clouds Media Group likiwa limeharibiwa kioo cha nyuma katika vurugu hizo.

 Hili ni moja ya makanisa matatu yaliyoharibiwa na waislamu wenye hasira kali leo jioni.

                                            Gari la polisi likiwa limeharibiwa katka vurugu hizo.

Haya ni maoni ya miongoni ya wadau wa mabadiliko katika ukurasa wake wa facebook juu ya tukio la leo anaitwa 'Mimi Mwanakijiji.'


 UKOSEFU WA HEKIMA NI JANGA KUBWA ZAIDI

Hii habari ni ishara ya matatizo makubwa zaidi. Hivi majuzi tumesikia kule Pakistan ambapo binti wa Kikritu nusura auwawe kwa sababu ilidaiwa kuwa alikufuru Quran kwa kuchana karatasi zake. Watu walikuja juu sana. Kumbe baadaye ikagundulika ni mzee mmoja wa Kiislamu ndiye aliyemset up yule mtoto ambaye ilidaiwa kuwa ana upungufu wa kiakili wa aina fulani. Baadaye ni yule Sheikh ndiye aliyekamatwa kwani ndiye aliyechana kurasa za Qurani na kuweka kwenye mfuko wa yule binti.

Sasa suala hili lina kila aina ya haja ya hekima. Unaposema kitabu hiki ni "kitakatifu" je mtoto anajua maana ya utakatifu? Je anajua hisia ambazo zinaendana na vitu hivi? Ni sawasawa na Wakatoliki wanaoamini komunyo ni kitu cha kiungu. Je mtoto wa dini nyingine anaweza kuelewa hili? Watoto wamekaa wanabishana kuhusu mambo ya vitabu hivi na mmoja anasema kitu ambapo akili ya kawaida haishawishiki; kwamba ukifanyia hivi basi unageuka panya. Mtoto yule mwingine udadisi umemshinda anasema 'haiwezekani'. Yule mwingine akiamini kabisa kuwa hilo hutokea akaenda kuchukua kitabu na kumletea huyu mwingine (vinginevyo huyo mtoto wa Kikristu alitoa wapi hiyo Quran?). Yule akajaribu na wote wakakaa hapo kuangalia kama atageuka mnyama. Hakugeuka!

Kama angegeuka kuwa panya yule mtoto mwingine angeelezeahilo tukio na badala yake eneo zima watu wangerindima kwa kisa cha mtoto aliyekojolea Quran ageuka panya! Sasa, haya mabishano yalikuwa ni ya kitoto na yasiyo nahekima yoyote. Watu wazima walipoitwa kuoneshwa kilichofanyika (kama ndivyo kilivyofanyika) walitakiwa kuonesha hekima ya kulishughulikia. Walitakiwa wawaeleweshe hawa watoto umakini na sensitivity ya vitu hivi na kwanini ni makosa kumtaka mtu akufuru kitabu cha Mungu ili uone nini kitamtokea na ni kosa pia kukubali jaribio hilo kwani linagusa imani za watu.

Hili jambo wala lisingefika hapa kabisa. Badala yake tunashuhudia mavuno ya mbegu ya udini. Mavuno ambayo watawala wetu wameyapanda na sasa hadi watoto wanavuna. Badala ya watoto wetu kuishi kwa kuaminiana na kupendana urafiki wao umetiwa mashakani na tukio hilo litaacha alama katika maisha yao yote. Na kama walikuwa ni marafiki wa karibu basi siyo tu wamepoteza urafiki kwa sababu ya ujinga wamejenga mpaka mpya kati ya Wakristu na Waislamu.

Yote haya ni kwa sababu ya kukosekana viongozi wenye hekima. Ndio maana binafsi ninalia sana na ukosefu wa hekima kama tunu ya muhimu zaidi kwa viongozi wetu. Leo watajaribu kutaka wananchi watulie kwa sababu sisi sote ni ndugu; lakini wakati mbegu za udini na chuki dhidi ya Wakristu zinapandwa kila siku wako kimya. Wanakuwa kimya pale ambapo Waislamu wanaona wanaonewa na kukandamizwa na mfumo wa kifisadi ambao wanaona umewabeba sana Wakristu! Matokeo yake ndiyo haya. Na tusipoangalia yatazidi kwa sababu endapo vijana wa Kikristu nao wakiamua kuchoma Misikiti au tutakuwa tumefika kule ambako niliwahi kuandika nyuma - Tanzania kufuata njia ya Nigeria.

Lakini cha kukwaza zaidi ni kuwa taarifa kwamba mtoto anayedaiwa kufanya hivyo kumbe ni Muislamu zinatosha kuthibitisha kuwa hekima inahitaji watu kutulia kwanza na kupata ukweli wote badala ya kupaparika na kuwahi kuhukumu watu. Sasa kama ni kweli mtoto aliyefanya hivyo ni Muislamu, hawa waliochoma makanisa wataenda na kuchoma misikiti? Au hawatochoma kwa sababu ni Muislamu "mwenzao"? Au wataamua kwenda kuchoma nyumba yake tu? Lakini watafanya nini kwa makanisa ambayo yamechomwa wwatasaidia na kujitolea kuyajenga tena baada ya kuyaharibu?

Kuna ugumu gani kwa watu kusubiri na kupata taarifa zote kwanza kabla ya kuchukua uamuzi wa kisheria au kisiasa (kuandamana n.k). Itakuwaje kama watu wangeuawa katika hili na baadaye igundulike kuwa ilikuwa ni watoto tu ambao walihitaji kuwekwa sawa tu? Kama kweli mtoto aliyefanya hivi ni Muislamu basi kilichotokea ni ushahidi usiopingika wa udini uliotukuka. Maana kusikia tu "mkristu kafanya hivi" basi Wakristu wote wamekwekwa hatiani!

Tuombe hekima zaidi kuliko kitu kingine kama alivyofanya Mfalme Suleiman (AS)

PICHA ZOTE KWA HISANI YA WWW.SAIDPOWA.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment