Thursday, October 11, 2012

SBC Tanzania Limited yangara tuzo za ubora wa viwango kimataifa.

Kutoka kushoto ni Michael Mafwenga meneja wa ubora wa viwango Pepsi, katikati ni Foti Nyirenda mkuu wa masuala ya mahusiano Pepsi na wa mwisho ni Separatus Kagashani ambae ni meneja wa kusimamia viwango vya ubora Pepsi.

Hizi ndizo tuzo zenyewe walizopewa na AIB International kuthibitisha ubora wa bidhaa za Pepsi.

Kutoka kushoto ni Michael Mafwenga meneja wa ubora wa viwango Pepsi na Separatus Kagashani ambae ni meneja wa kusimamia viwango vya ubora Pepsi, wakijivunia kazi yao. Maana hawa ndiwo wanaothibitisha ladha ya vinywaji vya Pepsi kabla havijaingia sokoni.



Hapa ndugu Nyirenda akisisitiza jambo kwa wanahabari wakati wa maswali na majibu.

Baada ya kazi namuona ndugu yangu Said Makala wa Channel Ten na Henry Mabumo (aliesimama) wa ITV wakijinafasi kwa vinywaji vya Pepsi na vitafunwa.


Na Hafidh Kido

Kampuni ya SBC Tanzania Limited wazalishaji wa kinywaji cha pepsi wametoa pongezi kwa wapenzi wa kinywaji hicho kwa kuwaunga mkono mpaka kuweza kupata tuzo nne za kimaifa za ubora na usalama zinazotolewa na AIB International.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam, mkuu wa masuala ya mahusiano SBC Tanzania Limited Foti Gwebe-Nyirenda, alisema kampuni yao imeweza kufikia hatua hiyo kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa wanywaji na wauzaji wa bishaa za Pepsi.

“Tunaahidi kuendelea kuwapa wanywaji na wateja wetu waaminifu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa wakati wote ili kuhakikisha wanaendelea kuthamini tuzo tuliyoipata kwa mwaka huu kwani ni heshima kubwa kwetu.

“Kampuni ya pepsi ipo dunia nzima hivyo Tanzania kuweza kushinda tuzo nne za kimataifa hiyo ni hatua kubwa na ya kuheshimika kuliko kawaida,” alisema Nyirenda.

Aidha SBC Tanzania Limited inayozalisha vinywaji vya Pepsi, Mountain Dew, Mirinda Orange, Mirinda Fruity, 7up na Evervess ilipata tuzo hiyo katika mkutano wa kimataifa uliofanyika nchini Dubai mwezi Agost 2012, katika nyanja za Utunzaji wa viwango vya ubora katika kuhifadhi bidhaa na kuwa miongoni mwa makampuni ya Pepsi duniani iliyofikia viwango vya juu katika Asia, Mashariki ya kati na ukanda wa Afrika.

Vilevile imeweza kutambuliwa katika tuzo ya kampuni bora inayotoa bidhaa bora kwa mwaka 2012 baada ya kufanyika ukaguzi na kampuni inayoongoza duniani kwa ukaguzi wa ubora ya AIB International.

Kampuni ya Pepsi imekuwepo nchini Tanzania kwa kipindi kirefu na kuweza kuendelea kutoa huduma ya vinywaji laini ambapo kwa sasa ndiyo inayoongoza barani Afrika kwa ubora wa bidhaa zake.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
11/10/2012

No comments:

Post a Comment