Wednesday, November 14, 2012

Abdulrahman Kinana Katibu mkuu mpya CCM... amuondoa Wilson Mukama..



Mkutano mkuu wa CCM umekamilika kwa Mwenyekiti Jakaya Kikwete kuteua watendaji wake wakuu, kikao kilichobakia sasa ni kile kitakachokaa na kujadili juu ya kupitisha majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa Chama kwa nafasi za wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya CCM, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe. Abdulrahaman Kinana .

Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
1.   Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
2.   Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Vuai Ali Vuai.
3.   Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
4.   Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
5.   Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
6.   Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.

kwa safu hii wabaya wa JK wameangukia pua, maana walioingia katika orodha hii wote ni watu wenye akili zao na wataongozwa na makamu mwenyekiti Bara ambae ni mwanasiasa mkongwe mwenye mrengo wa hayati baba wa Taifa Julius Nyerere ambae ni Philip mangula katibu mkuu wa zamani CCM.

Haya kazi iendelee….

No comments:

Post a Comment