Saturday, November 3, 2012

Jella Mtagwa soma kisa chake...


Pichani ni Stempu ya Shirika la Posta Tanzania ambayo imepambwa na Picha ya Mchezaji Mashuhuri wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania "Taifa Stars", Ndugu Jella Mtagwa.

Stempu hii ilitolewa na Shirika la Posta la Tanzania Mwaka 1982 na kuzua kizaazaa kikubwa sana kwa kuwa Mchezaji Mwenyewe Jella Mtagwa hakuhusishwa kabisa katika Mchakato Mzima wa Kutumia Picha yake katika Stempu hizi za Shirika la Posta.

Lakini sakata husika lilitulizwa na viongozi wa kilichokuwa Chama cha Soka nchini (FAT) wakati huo, Saidi El Maamry (mwenyekiti) na Marehemu Patrick Songora (katibu), ambao walimuelewesha Jella Mtagwa kwamba wao ndio waliotoa Idhini ya Picha yake kutumika kwenye Stempu hizo.

Shirika la Posta waliomba kwa chama hicho kiwapatie jina la mchezaji wanayeona anafaa picha yake kuwekwa kwenye stempu kama kivutio na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Viongozi hao wawili walimweleza Jella kwamba, waliamua kumpendekeza yeye kwa vile alitoa mchango mkubwa katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars kilichofuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 na pia alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 1981/1982.

Mpaka leo Shirika la Posta Tanzania halijawahi kumlipa Chochote Jella Mtagwa kwa kutumia Picha yake kwenye Matangazo ya Stempu zao.



Maelezo zaidi juu ya mwanasoka huyu nguli yanaeleza kuwa alianzia kucheza soka mjini Morogoro ambapo alinza na klabu ya Nyota morogoro, akacheza Pan African pamoja na Young African.

Historia yake inaeleza kuwa ndugu Jella alisoma shule ya msingi Mwembesono ya Morogoro, na katika mafanikio makubwa ni kuwa beki namba tano wa timu ya Taifa miaka hiyo.

Kwa sasa inaelezwa kuwa nguli huyu wa soka anasumbuliwa na maradhi ya kiharusi na hakuna hata kiongozi mmoja wa soka hata wale ambao alicheza nao soka miaka hiyo ambao kwa sasa wapo katika nafasi nzuri katika vyama vya soka akiwemo Rais wa TFF Leodger Tenga, Adolf Richard, Juma Pondamali ‘Mensah’.

Kidojembe itajitahidi kufanya utafiti zaidi na ikiwezekana kumtafuta nguli huyu na kufanya nae mahojiano ili kupata taarifa zake zaidi na ikiwezekana blogu hii imfuate mpaka kwake na kujua anaendelea vipi.

Mtu yeyote mwenye taarifa za nguli huyu, awasiliane na blogu hii ili tuweze kufika anapoishi. Shime Watanzania, Tutetee Haki na Maslahi Bora kwa Wachezaji. Uungwana ni Vitendo.


0713 593894/ 0752 593894
Kwa taarifa zaidi za namna hii like ukurasa wa ‘watanzania mashuhuri’ ilipopatikana taarifa hii.
Picha na Maelezo haya ni Sehemu ya Kampeni ya Ukurasa wa "Watanzania Mashuhuri"






No comments:

Post a Comment