Wednesday, November 28, 2012

Poleni wapenzi wa sanaa ya muziki na vichekesho...




 Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni


Hussein Mkiety 'Sharomilionea', amefariki usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari akiwa katika mji wa Muheza mkoa wa Tanga, siku chake kabla ya kifo chake, Sharomilionea alifanya mahojiano na mwanaspoti na kueleza mikakati yake mipya.

Akizungumza na mwanaspoti kabla ya kukutwa na umauti sharomilionea alisema kuwa hakuna mtayarishaji wa filamu kutoka Bongo Movie anayeweza kumlipa zaidi ya kumsifia tu kwamba anajua kuigiza.

Katika hali isiyo ya kawaida Sharomilionea alizungumza na mwandishi wa Mwanaspoti bila kujua kuwa amebakiza siku chache za kuishi hapa duniani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa muigizaji huyo maarufu wa vichekesho amefariki kwa ajali akiwa katika mkoa wa Tanga alikokwenda kikazi.

Kabla ya uhai wake muigizaji huyo nyota alizunguza na mwanaspoti na kuweka bayana mipango yake ya namna anavyoweza kuboresha zaidi fani yake hiyo ya vichekesho

Binafsi bado natafuta maisha, sipo kwa ajili ya kusifiwa ujinga huku wengine wakineemeka, naweza kusema Bongo Movie hakuna anayeweza kunilipa vizuri," alisema pasipokujua kuwa siku zake za kuishi zimekarinia.

"Mara nyingi sisi makomediani tunadharauliwa sana na baadhi ya watayarishaji, kwa hiyo hata malipo angetaka akulipe anavyotaka yeye huku akijiona kuwa yeye ni nyota."alifafanua siku chache kabla ya kifo chake

Msanii huyo alizidi kusema kuwa maisha yake ya sanaa hayakuwa rahisi kama inavyodhaniwa kwani amepitia katika changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kukataliwa kuigiza.

"Tena kuna ambao walikuwa wakinikatalia kuigiza nao, lakini sasa wananiomba nifanye nao kazi," anasema msanii huyo aliyeshirikishwa katika filamu ya mwisho ya Steven Kanumba 'Power & Love'.

Kwa masikitiko makubwa Tovuti hii ya Mwanaspoti inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Mungu aiweke roho ya mja wake mahali pema peponi.
Kwa habari zaidi endelea kufuatana nasi

No comments:

Post a Comment