Monday, November 26, 2012

Tigo ndiyo inayoongoza kwa malalamiko ya wateja....


Na: Waandishi Wetu, Hudumabongo@gmail.com

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi, Tigo imeshikilia usukani wa biashara inayoongoza kwa kero kwa wateja baada ya kuibuka kuwa mshindi miongoni mwa biashara 31 zenye kero kwa wateja nchini .

Taarifa hii ni matokeo ya zoezi linaloendeshwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wenye lengo la kuboresha sekta binfasi nchini Tanzania hususani huduma kwa wateja.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO mkoa wa Dar es Salaam ambao katika mzunguko wa kwanza ndiyo walishikilia usukani wa kero. Wakiongoza kwa kero ya kukata umeme bila taarifa kitu kinadaiwa kuwa ni mgao.

Nafasi ya tatu imeendelea kushikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo imeendelea kushika nafasi hiyo katika mzunguko wa pili.
Hakukuwa na mabadiliko katika makundi mengine mfano huduma za usafiri wa anga ambapo mshindi amebakia kuwa ni Precision Air, huku katika huduma za kibenki zikiendelea kushikiliwa na benki ya CRDB.

Huduma za ving’amuzi vya kulipia vyenye kero imeendelea kushikiliwa na Star Times waliopata kura 4 za ziada ukilinganisha na matokeo ya mzunguko wa kwanza.
Katika mzunguko huu biashara mbili zaidi ziliingia katika kinyanganyiro hicho ambao ni Kampuni mpya ya huduma za ndege ya Fast Jet na Dalalada inayofanya safari kati ya Mwenge na Kariakoo yenye nambari za usajili T 868 BHU.

Haya ni maoni ya wateja wa huduma hizi yaliyokusanywa kupitia akaunti ya twitter @hudumambayatz na Facebook group ya HUDUMA BONGO ambapo jumla ya kero 174 ziliwasilishwa na wateja toka mchuano uanze.

Zoezi la kukusanya maoni haya linaendelea katika mzunguko wa tatu ambapo kauli mbiu ya ni “Sisi ndio waajiri wenu , huduma bora ni haki yetu”. Kero katika huduma na bidhaa mbalimbali za kulipia mfano afya, elimu, usafiri, benki, mawasiliano zinapokelewa na kutafutiwa suluhisho kwa maendeleo ya taifa letu.

Kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea link ifuatayo http://bit.ly/10SARH1


No comments:

Post a Comment