Wednesday, January 9, 2013

Ayew Pele aachwa katika kikosi cha Ghana kitakachokwenda Afrika Kusini.



Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ghana Kwesi Appiah, amemuondoa Andre 'Dede' Ayew katika kikosi chake kitakacho shiriki katika michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Ayew, alikosa kufika kambini Abu Dhab kutokana na jeraha la paja, ambalo bado halijathibitishwa na madaktari wa timu hiyo.
Mcheza kiungo huyo aliruhusiwa na klabu yake ya Ufaransa ya Marseille, ili ajiunge na timu hiyo ya taifa ya Ghana, kufuatia ombi lililowasilishwa kwa klabu hiyo na shirikisho la mchezo huo nchini Ghana.
'' Nimeamua kumuacha nje ya kikosi changu kitakacho elekea Afrika Kusini'' Alisema Appiah.
Chini ya sheria za FIFA, vilabu vya soka vinapaswa kuwaruhusu wachezaji siku ya Jumamosi, wiki mbili kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini.
Vilabu pia ni shartiw aruhusu wachezaji waliojeruhiwa kuchunguzwa na madaktari wa timu zao za taifa.
''Andre hakujitokeza, licha ya kuwa tayari alikuwa amepewa idhini na klabu yake na pia kukabithiwa tikiti ya ndege ya shirikisho la mchezo wa soka la Ghana, ili asafiri kutoka Ufaransa hadi kambini'' Kocha huyo aliongeza.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa hakufika kambini na kusema kwamba hakuwa amemaliza matibabu aliyokuwa akipewa na daktari wake ili afike kambini siku ya Jumatano, tarehe 9 mwezi huu.
''Mchezaji huyo aliamriwa kufika kambini siku ya Jumatatu kwa kuwas siku ya Jumatano ndio siku ya mwisho kwa nchi mbali mbali kuwasilisha majina ya wachezaji wake kwa shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF.
Appiah kwa sasa ana kikosi cha wachezaji 25 na ni sharti apunguze kikosi hicho kabla ya siku ya Jumatano, wakati atakapotaja rasmi kikosi kitakacho akilisha Ghana kwenye faianli hizo.
Ghana inaanza kampeini yake ya fainali hizo za Afrika tarehe 20 Januari dhidi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kabla ya kucheza na Mali na Niger katika kundi B.

No comments:

Post a Comment