Tuesday, January 1, 2013

Haya jamani kwa wenye magari EWURA wametangaza punguzo la bei ya mafuta....


KUMB: PPR/13 - 1/1
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI  KUANZIA
JUMATANO, TAREHE 2 JANUARI 2013

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza  bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 2 Januari 2013. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo.

(a)                Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 05 Desemba 2012. Katika toleo hili, bei za rejareja kwa  Petroli,  Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 126/lita sawa na asilimia 5.96; Dizeli Sh 32/lita sawa na asilimia 1.60; na Mafuta ya Taa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.50. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo  haya  mawili zimepungua kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 126.10/lita sawa na asilimia 6.17; Dizeli kwa Sh 32.48/lita sawa na asilimia 1.69; na Mafuta ya Taa kwa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.6. Mabadiliko haya ya bei yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

(b)                Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(c)                Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.

(d)                Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

(e)                Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

A: BEI ZA REJAREJA


Bei Kikomo
Mji
Petroli
Dizeli
Mafuta ya Taa

(Tsh/Lt)
(Tsh/Lt)
(Tsh/Lt)
Dar es Salaam
1,993
1,967
1,973
Arusha
2,077
2,051
2,057
Arumeru (Usa West)
2,077
2,051
2,057
Karatu
2,095
2,069
2,075
Monduli
2,082
2,056
2,062
Ngorongoro (Loliondo)
2,133
2,107
2,113
Kibaha
1,997
1,972
1,977
Bagamoyo
2,004
1,978
1,984
Kisarawe
2,000
1,974
1,980
Mkuranga
2,002
1,977
1,982
Rufiji
2,020
1,995
2,000
Dodoma
2,051
2,026
2,031
Bahi
2,059
2,033
2,039
Chemba
2,078
2,052
2,058
Kondoa
2,084
2,058
2,064
Kongwa
2,049
2,023
2,029
Mpwapwa
2,052
2,027
2,032
Iringa
2,057
2,031
2,037
Kilolo
2,061
2,035
2,041
Mufindi (Mafinga)
2,067
2,041
2,047
Njombe
2,085
2,059
2,065
Ludewa
2,123
2,097
2,103
Makete
2,116
2,090
2,096
Wanging'ombe (Igwachanya)
2,083
2,057
2,063
Bukoba
2,208
2,182
2,188
Biharamulo
2,182
2,156
2,162
Karagwe (Kayanga)
2,224
2,198
2,204
Kyerwa (Ruberwa)
2,230
2,204
2,210
Muleba
2,208
2,182
2,188
Ngara
2,173
2,147
2,153
Misenyi
2,216
2,190
2,196
Geita
2,158
2,132
2,138
Bukombe
2,147
2,121
2,127
Chato
2,179
2,153
2,159
Mbogwe
2,196
2,170
2,176
Nyang'hwale
2,173
2,147
2,153
Kigoma
2,223
2,198
2,203
Uvinza (Lugufu)
2,236
2,210
2,216
Buhigwe
2,213
2,187
2,193
Kakonko
2,181
2,155
2,161
Kasulu
2,210
2,184
2,190
Kibondo
2,188
2,162
2,168
Moshi
2,066
2,041
2,046
Hai (Bomang'ombe)
2,069
2,044
2,049
Mwanga
2,059
2,034
2,039
Rombo (Mkuu)
2,087
2,061
2,067
Same
2,053
2,027
2,033
Siha (Sanya Juu)
2,073
2,047
2,053
Lindi
2,051
2,026
2,031
Kilwa Masoko
2,026
2,001
2,006
Liwale
2,072
2,047
2,052
Nachingwea
2,081
2,055
2,061
Ruangwa
2,079
2,053
2,059
Babati
2,115
2,089
2,095
Hanang (Katesh)
2,125
2,100
2,105
Kiteto (Kibaya)
2,126
2,100
2,106
Mbulu
2,127
2,102
2,107
Simanjiro (Orkasumet)
2,147
2,121
2,127
Musoma
2,171
2,145
2,151
Rorya (Ingirijuu)
2,180
2,154
2,160
Bunda
2,162
2,136
2,142
Butiama
2,168
2,142
2,148
Serengeti (Mugumu)
2,216
2,191
2,196
Tarime
2,182
2,156
2,162
Mbeya
2,099
2,074
2,079
Chunya
2,109
2,083
2,089
Ileje
2,113
2,087
2,093
Kyela
2,115
2,090
2,095
Mbarali (Rujewa)
2,084
2,058
2,064
Mbozi (Vwawa)
2,109
2,083
2,089
Momba (Chitete)
2,118
2,092
2,098
Rungwe (Tukuyu)
2,108
2,083
2,088
Morogoro
2,018
1,992
1,998
Mikumi
2,033
2,008
2,013
Kilombero (Ifakara)
2,055
2,030
2,035
Ulanga (Mahenge)
2,066
2,040
2,046
Kilosa
2,036
2,010
2,016
Mvomero (Wami Sokoine)
2,028
2,002
2,008
Mtwara
2,065
2,039
2,045
Nanyumbu (Mangaka)
2,114
2,088
2,094
Masasi
2,090
2,065
2,071
Newala
2,097
2,071
2,077
Tandahimba
2,090
2,064
2,070
Mwanza
2,142
2,117
2,122
Kwimba
2,178
2,153
2,158
Magu
2,150
2,125
2,130
Misungwi
2,148
2,122
2,128
Sengerema
2,175
2,149
2,155
Ukerewe
2,202
2,176
2,182
Sumbawanga
2,165
2,139
2,145
Kalambo (Matai)
2,158
2,132
2,138
Nkasi (Namanyele)
2,179
2,153
2,159
Katavi (Mpanda)
2,200
2,174
2,180
Mlele (Inyonga)
2,178
2,153
2,158
Songea
2,116
2,090
2,096
Mbinga
2,149
2,124
2,129
Namtumbo
2,145
2,119
2,125
Nyasa (Mbamba Bay)
2,152
2,126
2,132
Tunduru
2,175
2,149
2,155
Shinyanga
2,121
2,096
2,101
Kahama
2,135
2,109
2,115
Kishapu
2,150
2,124
2,130
Simiyu (Bariadi)
2,163
2,137
2,143
Busega (Nyashimo)
2,156
2,130
2,136
Itilima (Lagangabilili)
2,166
2,140
2,146
Maswa
2,154
2,128
2,134
Meatu (Mwanhuzi)
2,161
2,135
2,141
Singida
2,083
2,057
2,063
Iramba
2,095
2,070
2,075
Manyoni
2,068
2,042
2,048
Ikungi
2,079
2,053
2,059
Mkalama (Nduguti)
2,108
2,082
2,088
Tabora
2,147
2,121
2,127
Igunga
2,101
2,075
2,081
Kaliua
2,165
2,139
2,145
Ulyankulu
2,159
2,133
2,139
Nzega
2,111
2,085
2,091
Sikonge
2,158
2,133
2,138
Urambo
2,160
2,134
2,140
Tanga
2,039
2,013
2,019
Handeni
2,018
1,992
1,998
Kilindi
2,053
2,027
2,033
Korogwe
2,032
2,006
2,012
Lushoto
2,041
2,016
2,021
Mkinga (Maramba)
2,053
2,027
2,033
Muheza
2,039
2,013
2,019
Pangani
2,045
2,020
2,025








B: BEI ZA JUMLA


Bei za Jumla - DSM
Petroli (Sh/L)
Dizeli  (Sh/L)
Mafuta ya Taa (Sh/L)
Bei Kikomo
1,918.60
1,892.97
1,898.62







Haruna Masebu
MKURUGENZI MKUU
  EWURA




































No comments:

Post a Comment