Saturday, January 19, 2013

Je Unajua matajiri 100 tu waliopo duniani wanaweza kulisha maskini wote?


Shirika la msaada la kimataifa, Oxfam, linasema kuwa watu 100 tajiri kabisa duniani walipata fedha za kutosha mwaka jana za kuweza kumaliza ufukara wa watu maskini kabisa duniani, mara nne zaidi.

Oxfam inasema kuwa mwaka jana pato la matajiri wakubwa kabisa 100 lilikuwa jumla ya dola 240 bilioni.
Na watu maskini kabisa wanatumia dola moja na robo tu kwa siku.
Katika taarifa iliyotoa kabla ya mkutano wa kiuchumi wa Davos, Usiswi, juma lijalo, Oxfam imesema kuzidi kwa utajiri mkubwa duniani unazuwia juhudi za kupambana na umaskini.

No comments:

Post a Comment