Tuesday, January 1, 2013

Kumbe Messi hajavunja rekodi ya kufunga mabao mengi, Godfrey Chitalu wa Zambia alifunga mabao 107 katika mwaka 1972..

Shirikisho la soka la Zambia, linasema linataka shirikisho la soka duniani FIFA kutambua mcheza soka wa nchi hiyo Godfrey Chitalu kwa uhodari wake wa kuingiza mabao 107 mnamo mwaka 1972.
Hatua hii inakuja baada ya gwiji wa soka Lionel Messi kuvunja rekodi ya mcheza soka mjerumani Gerd Mueller aliyeingiza mabao 85 katika mwaka mmoja. Messi sasa ameingiza mabao 88 mwaka huu (mwaka jana) pekee.
Msemaji wa shirikisho la soka la Zambia, Faz, Eric Mwanza, aliambia BBC kuwa wana rekodi za kuthibitisha kuwa Chitalu anapaswa kutambuliwa kwa mabao aliyoingiza.
''Tunataka kusema wazi kuwa sio swala la kuthibitisha madai yetu au kujaribi kuhakikisha kuwa ni kweli aliingiza mabao hayo, hakuna utata kuhusu hili.'' alisisitiza bwana Mwanza.
Kile ambacho tunahoji hapa ni kwa nini hajatambuliwa na hicho ndicho sisi tunataka''
"tunamtumia ujumbe, katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, kuangalia upya swala hili la Godfrey Chitalu."
Baada ya maisha yake kama mchezaji wa soka, Chitalu alichukua wadhifa wa kocha na hivyo kuanzisha timu ya taifa ya Zambia.
Alifariki pamoja na wachezaji wengine 29, 18 miongoni mwao wakiwa wachezaji wa kimataifa, katika ajali ya ndege katika pwani ya Gabon walipokuwa wanakwenda Senegal kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia.
Mwanza pia aliongeza kuwa mwaka 1972, haikuwa ndio mara ya kwanza kwa Chitalu kucheza vizuri kabisa.
"katika msimu wa ligi kabla ya mwaka 1972, aliingiza mabao 89 ," bwana Mwanza alielezea zaidi.
Mnamo mwaka 1972, aliingiza mabao 107, yaliyohusisha mechi za ligi , mechi za vilabu , mechi za kitaifa pamoja na mechi za kirafiki''
Rais wa Faz, Kalusha Bwalya, alisema kuwa anakumbuka vyema sana alivyocheza bwana Chitalu.
''Kwa hivyo ingekuwa muhimu sana kumtambua kwa umahiri wake wa kuingiza mabao,'' alisema Bwalya
"baadhi yetu tumeona wachezaji kama Pele, Platini, Maradona na Van Basten, kama chezaji wa zamani wa soka, siku hizi, ni vigumu sana kuingiza mabao 20, kwa hivyo asalie kusifiwa Messi.
Mtandao mmoja wa nchini Zambia unadai kuwa Chitalu aliingiza mabao 116 mwaka 1972, lakini haijazingatia mabao tisa ya kwanza aliyoingiza katika mechi za kilabu bingwa Afrika
Chanzo: BBC Swahili…

No comments:

Post a Comment