Tuesday, January 1, 2013

Mapinduzi Cup hii ndiyo ratiba wadau....

Mabingwa watetezi kombe la Mapinduzi Azam FC.......


Suleiman Kassim 'Selembe' mchezaji wa kutumainiwa Coastal Union ambae chama cha soka cha Zanzibar ZFA kimemfungia kucheza soka kutokana na kutorudisha mgao wa washindi wa tatu Challenge Cup haijulikani kama atakuwepo katika kikosi.





Ratiba ya michuano ya kombe la mapinduzi imetoka na mchezo wa kwanza utaanza kurindima kesho usiku mbele ya makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Seif Sharif hamad.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa kamati ya maandalizi Farouk Karim ‘Zidane’ amesema ufunguzi huo utakuwa saa mbili usiku katika uwanja wa Aman mjini Unguja ambapo Simba na Jamhuri ya Pemba zitamenyana kuonyeshana nani ataanza na nuksi katika michuano hiyo inayofanyika kila mwaka kuadhimisha mapinduzi yaliyiofanyika mwaka 1964.

Aidha mchezo wa pili utakuwa saa kumi alasiri siku inayofuata katika uwanja wa Mao Tse Tung timu ya Mtibwa kutoka Turiani Morogoro itashuka dimbani dhidi ya Miembeni ‘watoto wa mjini’ kutoka unguja. Halkadhalika januari 4 timu ya Jamhuri itakipiga na  Bandari majira ya saa kumi alasiri ambapo Tusker ya Kenya itamenyana na Simba usiku saa mbili.

Januari 5 Mtibwa Sukari itakipiga na Coastal Union ‘wagosi wa kaya’ kutoka Tanga saa kumi alasiri, wakati usiku saa mbili Miembeni itakabiliana na Azam FC. Mechi nyingine itakuwa baina ya Tusker na Jamhuri saa kumi alasiri na Simba watakipiga na Bandari saa mbili usiku.

Katika kuhitimisha kundi B Coastal Union itakabiliana na Miembeni saa kumi alasiri  wakati saa mbili usiku Azam FC watahitimisha na Mtibwa sukari.

Nusu fainali itachezwa januari 9 na januari 10 mechi zote zitachezwa usiku. Wakati siku ya kilele cha sherehe za mapinduzi yaani januari 12 ndipo fainali itakapochezwa katika uwanja wa Amani saa mbili usiku.

Group A: Simba SC, Tusker FC, Bandari (Unguja) and Jamhuri (Pemba). 
Group B: Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union, and Miembeni (Unguja)
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
+255 752 593894/ +255 713 593894
kidojembe@gmail.com

No comments:

Post a Comment