Monday, January 14, 2013

Wanafunzi wa Chuo cha IFM wapinga wenzao wawili kulawitiwa... tukio hili linaendelea huko kigamboni hivi tunavyozungumza....

 Hapa wanafunzi wa IFM wakiandamana kupinga wenzao wawili kuvamiwa na majambazi halafu wakalawitiwa. Wamekwenda ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi kupeleka malalamiko yao kuwa waliwahi kuripoti kukosa usalama katika mabweni ao ila jeshi hilo halijachukua hatua zozote.

 Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha IFM wakiwa ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi nchini jijini Dar es salaam leo mchana.

 Kiongozi wa wananfuzi iFM akimweleza kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam Suleiman Kova juu ya kadhia iliyowapata wenzao kwa kuvamiwa na majambazi wakiwa wamelala.

Baada ya kuzungumza nao kamanda Kova aliamua kuandamana nao mpaka zilipo Hostel na kituo cha polisi walichodai waliripoti matatizo yao lakini hawakusikilizwa. Kova aliwaahidi watapanda kivuko bila malipo, tatizo wanafunzi walijaa kuliko uwezo wa kivuko. Hapa akijadiliana na askari wenzie namna ya kuwapunguza wanafunzi hao....


Wanafunzi hao walivamia makao makuu ya jeshi hilo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.

Picha zote kwa hisani ya blog ya Said Powa.
Maelezo kidojembe.
fuatilia habari hii jioni itakuwa imekamilika tunasuburi taarifa zaidi kutoka blog ya mwanajamii Said Powa.

No comments:

Post a Comment