Tuesday, February 19, 2013

Juhudi za January Makamba zaifanya Bumbuli kuwa Halmashauri ya wilaya.



Hatimaye suala nililolipigania kwa miaka miwili limefanikiwa. Jimbo la Bumbuli sasa limepata Halmashauri ya Wilaya. Kwa mfumo wa mfumo wa utawala wa nchi yetu, maendeleo yanapangwa, kusimamiwa na kutekelezwa katika ngazi ya Halmashauri. Baada ya kujing'atua kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, sasa tutakuwa na rasilimali nyingi zaidi za maendeleo, tutakuwa na eneo dogo zaidi la usimamizi wa shughuli za maendeleo (tulipokuwa ndani ya Halmashauri ya Lushoto tulikuwa Kata 44, sasa tutakuwa Kata 16 tu), tutasogeza huduma za kiutawala na kijamii karibu zaidi na watu, na tutasukuma maendeleo kwa kasi zaidi. Kazi iliyo mbele yetu sasa ni kuisimamia vizuri hii Halmashauri ili malengo yetu yatimie. Kazi hiyo tutaifanya. Tunaizindua Halmashauri hii tarehe 24 Februari 2013. Nyote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment