Thursday, February 7, 2013

kidojembe inatoa pole kwa wakristo wote wa madheheb ya kkkt Tanzania kwa msiba wa Askof Laizer Thomas...


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini.Askofu Thomas  Laizer amefariki duniaalasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha. Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
alimtembelea  na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.
Pinda alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye.


No comments:

Post a Comment