Monday, March 11, 2013

JK amekumbuka wazee wanamichezo tu wiki hii...

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo  leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili, atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia amefundisha nyota wengi wa  kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard, Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa Stars kutokea Yanga na Pan..

 Baada ya kushiriki mazishi huyoooo akaanya safari mpaka Ikulu.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.
Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtaki apate nafuu ya haraka.

PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment