Saturday, March 9, 2013

Kibanda amweleza Rais Kikwete namna alivyovamiwa...

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg,  Afrika ya Kusini leo jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).



Rais Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ambaye pia ni kiongozi wa ANC (Watatu kushoto),Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC.

(picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment