Tuesday, March 5, 2013

Kura nyingi zimeharibika uchaguzi Kenya...


Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, imesema ina wasi wasi kuhusu idadi ya kura zilizoharibika na imesema italazimika kuchunguza kisa cha idadi kubwa ya kura kuharibika.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Ahmed Issack Hassan, amesema kuwa uchunguzi utafanywa mwishoni mwa uchaguzi kujua kwa nini wapiga kura walifanya makosa makubwa wakati wa upigaji kura.
Hizi ni kura mara mbili ya kura alizopata mgombea wa urais wa muungano wa Amani , Musalia Mudavadi zikijumulishwa na kura walizopata wagombea wengine waliokuwa na kura chache kumliko hadi kufikia sasaWakati tume hii ilikuwa inatoa taarifa kuhusu kura hizo, takriban kura 284,232 zilikuwa zimeharibika.
''Ni kweli hii ni idadi kubwa sana ya kura zilizoharibika,''alisema bwana Hassan. Hizi ndizo kura zilizopigwa na ambazo sasa zimeharibika.....aidha kwa sababu ziliwekwa alama isiyostahili.''
Alisema Hassan wakati wa shughuli hiyo tume iligunduwa kuwa kuna mahali ambapo wapigha kura waliweka karatasi za kura katika masunduku yasiyostahili.
Bwana Hassan alisema kuwa huenda rangi ziliwachanganya watu kwani hazikuwa na nguvu sana, kama mfano rangi ya kijani kibichi haikuwa kama ilivyostahili kuwa
Aliongeza kuwa huenda tatizo hili linatokana na ugumu wa upigaji kura ambapo wapiga kura walikuwa wanachagua wagombea sita wakiwemo, wabunge , waakilishi wa wanawake, maseneta, magavana , waakilishi wa wodi na rais.
Alisema kuwa sababu ya kuharibika kwa kura itatolewa baada ya uchunguzi kamili kufanywa pamoja na maoni ya maafisa waliosimamia uchaguzi huo.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment