Wednesday, March 6, 2013

Mohammed Gharib Bilal amtembelea Absolom Kibanda wodi ya MOI.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, aliyelazwa katika Wodi ya Moi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana wakati akiingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. 

Pembeni alievaa miwani ni Said Kubenea aliekuwa mhariri wa Mwanahalisi, ambalo kwa sasa limefungiwa na Serikali. Kubenea nae aliwahi kumwagiwa tindikali akiwa ofisi za Mwanahalisi miaka ya nyuma na kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Picha na Ofisi ya Mamaku wa Rais

No comments:

Post a Comment