Wednesday, March 6, 2013

Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia.



Aliugua saratani kwa muda mrefu na kufanyiwa upasuaji nchini Cuba, jambo lililomfanya asionekane hadharani kwa miezi kadhaa.
Rais Obama , ambaye nchi yake imekuwa na uhusiano mgumu na rais Chavez amezungumzia juu ya kipindi cha changamoto kinachoikabili Venezuela na kuongeza kuwa Marekani itatoa msaada kwa watu wa Venezuela.
Balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitaly Churkin amesema kuwa bwana Chavez amekuwa mwanasiasa shupavu kwa nchi yake , kwa eneo la Amerika ya kusini na dunia kwa ujumla.
Naye rais wa Argentina , Cristina Fernandes de Kirchner, amesema kuwa ameakhirisha shughuli zake zote baada ya kusikia taarifa ya kifo cha rafiki na mshirika wake .
Rais wa Cuba Fidel Castro amesema anaomboleza kifo cha mtu ambaye alikuwa kama kijana wake.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment