Sunday, March 17, 2013

Ripoti ya maendeleo ya watu Duniani....


Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwapokea wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wanafunzi wa vyuo vikuu, Maprofesa, na wadau wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 uliofanyika jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.

 Uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya watu Duniani mwaka 2013 katika hoteli ya Serena leo.

 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 –

Mabalozi na viongozi mbalimbali wakipitia ripoti hiyo iliyozinduliwa leo na ofisi ya umoja wa mataifa- Tanzania.


Kuchomoza kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa mujibu wa ripoti hii mwaka huu inaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti iliyopita.Hata hivyo amesema kuwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima ujumla wa maendeleo katika Jamii. Bw. Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.

Habari na picha kwa hisani ya Zainul Mzige wa Mo Blog



No comments:

Post a Comment