Tuesday, March 5, 2013

Tume ya uchaguzi Kenya yakiri hitilafu za mitambo...




Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya imekiri kuwa kulikuwa na hitilafu chungu nzima za kimitambo, katika kutoa matangazo ya matokeo ya kura za urais kutoka kwa vituo vya kupigia kura kote nchini.
Afisaa mkuu mtendaji wa tume hiyo,James Oswago alielezea kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na kiasi kikubwa cha matokeo yaliyokuwa yanapeperushwa moja kwa moja kutoka kwa vituo vya kupigia kura kwa sababu ya ukosefu wa nafasi ya kutosha kwenye mitambo yake.
Akihutubia waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas ambako matokeo ya urais yanatarajiwa kutangazwa, Bwana oswago alisema kuwa tume hiyo iliweza kurekebisha mitambo yake.
Pia aliongeza kuwa maajenti wa wagombea wote wakuu wawili walifahamishwa kuhusu hutilafu hiyo.
Kugoma kwa muda kwa mitambo ya kupeperusha matokeo, ilisababisha hali ya wasiwasi, baada ya IEBC kusitisha kupeperusha matangazo kwa masaa kadhaa.
Maafisa wa Miungano yote ya Jubiliee na CORD, walitetea kwa sababu ya kucheleweshwa kwa matokeo na kulaumu tume ya IEBC, baada ya maafisa wake wote kuondoka katika ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais.
Kamishna mmoja mkuu wa tume hiyo aliwataka watu kuwa watulivu akisema hakuna sababu ya watu kuwa na wasiwasi.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment