Monday, March 25, 2013

Wachezaji TP Mazembe waibeba Stars...


Mabao matatu ya nyota wa TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu yalitosha kuipa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Morocco katika mechi ya kutafuta tik-eti ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia, Brazil 2014.

Kwa ushindi huo, Stars sasa imefikisha pointi sita na hivyo kuendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C ikiwa nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, baada ya kuifunga Gambia mabao 3-0 juzi.

Mshambuliaji Ulimwengu aliyeingia akitokea benchi kipindi cha pili alifunga bao la kwanza la Stars dakika ya 46, kabla ya kumtengenezea nyota mwenzake wa TP Mazembe, Samata aliyefunga men-gine mawili dakika ya 66 na 80.

Stars ilianza mchezo huo kwa kasi na kulifikia lango la wapinzani wao dakika ya pili tu ya mchezo wakati shuti la kiungo Amri Kiemba ilipogonga mtambaa wa panya kabla ya mabeki wa Morocco kuon-doa mpira kwenye hatari.

Dakika ya tisa Morocco ilijibu mapi-go na kona iliyochongwa na Barrada Abdellaziz ilimfikia Abuurazouk Hamza ambaye alipiga kichwa kilichotoka senti-mita chache kwenye lango la Stars.

Baada ya kashikashi hizo, kila upande ulijaribu kutuliza mpira chini na kupelekeana mashambulizi kwa zamu. Hata hivyo hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna timu ili-yokuwa imetingisha nyavu.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kuz-induka upya na kupeleka mashambulizi kuelekea kwa wapinzani wao Morocco na kupata bao dakika moja tu kupitia kwa Ulimwengu, ambaye ulikuwa ni mpira wake wa kwanza kuugusa.

Ulimwengu aliyeingia uwanjani kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mwinyi Kazi-moto alipachika bao hilo kwa shuti kali la karibu lililomshinda kipa wa Morocco, Lamyaghir Nadir kutokana makosa ya mabeki wake waliochelewa kuondosha mpira kwenye eneo lao la hatari.

Samata ambaye takriban muda wote wa mchezo alikuwa kero kwa mabeki wa Morocco alifunga bao lake la kwanza kwa shuti la pembeni baada ya kuwa-toka mabeki wa Morocco kisha kufunga lingine kwa kumalizia pande la kukata la Ulimwengu.

Dakika ya 81, mwamuzi wa mchezo huo Helder Martins kutoka Angola alim-wonyesha kadi nyekundu Achachakir Abdelkarim wa Morocco baada ya kum-tolea lugha chafu na kumsukuma aki-dai alitendewa faulo na Ulimwengu kabla hajatoa pasi ya bao kwa Samata.

Katika mechi hiyo, kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 64, kwa kumtoa Ngasa nanafasi yake kuchukuliwa na Athumani Iddi, pia dakika ya 89 alimtoa Samata na kum-wingiza John Bocco.

Dakika ya 90, Chaeni Kamal alifunga bao la kufuatia machozi kwa upande wa Morocco na hivyo kufanya matokeo kuwa 3-1. Akizungumza baada ya mechi kumal-izika, kocha Kim alisema: “Nimefurahish-wa na ushindi huu, vijana wangu waliji-tuma na wanastahili ushindi, ninaomba Watanzania waendelee kuiunga mkono Taifa Stars.”
Alisema: “Kipindi cha kwanza Moroc-co walikuwa wakijilinda na kufanya mashambulizi ya kushtukiza huku wakitegemea pia mipira iliyokufa.”
Chanzo: Mwananchi.

No comments:

Post a Comment