Thursday, April 4, 2013

Askofu wa zamani wa kanisa la Anglikana Afrika Kusini katika jimbo la Cape Town Desmond Tutu, ametajwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Templeton ambapo atapokea kima cha Dola milioni 1.6

Desmond Tutu mtetezi haki za wanyonge



Tutu mwenye miaka 87 ametaja Tuzo hii kama ushindi kwa wote wanaotetea haki za wanyonge bila kubagua.
Askofu Tutu atapokea tuzo hiyo mwezi ujao mjini London, Uingereza.
Akijibu ushindi huo mwanaharakati huyo wa haki za binadamu amesema kwamba jamii huwatuza wote wanaotetea haki yao.
Tuzo hii ilianzishwa mwaka wa 1972 kutolewa kwa raia ambao huchangia zaidi masuala ya imani na dini bila ubaguzi, ambaye pia hutetea haki za wanyonge.
Mwasisi wa tuzo hii Sir John Templeton alikua raia wa Marekani lakini akahamia Uingereza ambapo pia alituzwa na Malkia kwa mchango wake kwa jamii mwaka 1987.
Alifariki dunia mwaka 2008.Mwaka jana Tuzo ya Templeton ilitolewa kwa Kiongozi wa Kiroho wa Tibet Dalai Lama.
Mwaka jana Askofu Tutu alipokea dola Milioni moja kutoka kwa Wakfu wa Mo' Ibrahim ambayo hutoa tuzo kwa raia waafrika ambao hutetea haki na ukweli na kutetea utawala bora.
Desmond Tutu alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984 kutokana na harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Chanzo: BBC Swahili.


No comments:

Post a Comment