Wednesday, April 24, 2013

Bondia Star Boy kucheza pambano la utangulizi siku ya Mei Mosi, wakati wa pambano la Cheka na Mashali.


1 416b2
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' katika kambi ya Ilala iliyopo Amana CCM jana Sta Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
2 b1711
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
3 cc70f
Shabani Mhamila 'Star Boy'
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' anaendelea kujifua kwa ajili ya kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi kwenye mchezo kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.

Kwenye pambono hilo la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu kila mmoja amejigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa kumchakaza Jibaba ili kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na Mashali" alisema Super D na kuongeza Star Boy alishawahi kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na hali ya maisha lakini kwa sasa ameamua kurudi katika masumbwi ili kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi kutojui sheria na kanuni za mchezo huo.

Star Boy mwenye rekodi ya kucheza mapambano 23, akiwa ameshinda mapambano 14 (KO 5), na kupoteza 7 (KO 4) huku akitoa suluhu mbili.

Mkanda wa kwanza wa taifa kwa bondia Sta Boy alichukua Februari 2,1996 kwa kumtwanga bondia Theodor Luanda na kuutetea vema Februar1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa.

Aidha kocha Super D alisema katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila,Japhet Kaseba,Hassani Matumla,Rashidi Matumla dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' pamoja na mabondia mabingwa wa dunia
 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

No comments:

Post a Comment