Tuesday, April 16, 2013

Chama tawala nchini Uganda cha National Resisitance Movement-NRM- kimewafukuza baadhi ya wanachama wake wanne, wote wakiwa ni wabunge, kwa kile kilichoitwa utovu wa nidhamu.




Mbunge mwingine yeye amesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu kwa sababu za ulevi.Katibu mkuu wa chama hicho Amama Mbabazi anasema hii kwa tafsiri yake inamaanisha kuwa wabunge hao wamepoteza viti vyao, jambo ambalo wahusika wanapinga.
Katibu mkuu wa chama tawala cha NRM na wakati huo waziri Mkuu wa Uganda,Amama Mbabazi, ametangaza maamuuzi ya kamati kuu ya chama hicho kuhusu majaliwa ya wabunge wanne waliopewa jina la ‘wabunge waasi’ kutokana na misimamo yao dhidi ya masuala mbalimbali katika chama hicho.
Mbabazi alitoa kauli hiyo na kusema, ''Muhammad Nsereko afukuzwe kutoka NRM;kuwa Theodor Sekikubo afukuzwe kutoka NRM;kuwa Barnabas Tinkasimire afukuzwe kutoka NRM;kuwa Wilfred Nuwagaba wamefukuzwe kutoka NRM; na kuwa Vicent Kyamadidi Muzuni asimamishwe uana chama wa NRM kwa muda wa miezi mitatu.''
Wabunge wanne waliofukuzwa kutoka chama:Nsereko;Sekikubo;Tinkasimire pamoja na Niwagaba wamekuwa wakipinga na kukosoa saana uongozi wa sasa wa chama hususan kutokana na madai ya ufisadi dhidi ya vigogo wa chama.

Na wanasema hatua hii ni ya kuwaandama kisiasa kwa kusema ukweli dhidi ya wanachoita uongozi mbaya. Hatua ya kuwafukuza wanachama hao , inasekena ni kutokana na utovu wa nidhamu.

Wabunge hao walishtakiwa katika kamati ya nidhamu ya chama na kukabiliwa mashataka saba: kuwapigia debe wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mdogo; kupaka matope wagombea rasmi wa chama cha NRM wakati wa uchaguzi mdogo; kutoa madai ya uongo kwa vombo vya habari dhidi ya chama cha NRM; kutumia majukwaa haramu, kama vile vyombo vya habari na mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kuzungumzia masuala yanayowakera;kujihusisha katika uundaji wa genge ndani mwa NRM; matumizi ya lugha chafu;na mwisho kukaidi kamati ya nidhamu ya chama.Wote licha ya kuwaita kufika mbele ya kamati hiyo kujieleza walipinga.
Hii ndiyo mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi kuanza tena mwaka wa 2006, chama cha NRM kufukuza wanachama wake.
Na hii imezusha tafsiri tofauti kwa wabunge wanaofukuzwa chama.Katibu mkuu wa NRM anasema kuwa hii inamaanisha kuwa wamepoteza viti vyao vya ubunge.
Mbabazi aliongeza kusema kuwa ''Kulingana na sheria za Uganda, hususan kifungu 83 cha katiba ya taifa ni kuwa mtu anaweza kuwa mbunge pindi tu ikiwa amechaguliwa kama mbunge wa kujitegemea,au ikiwa amechaguliwa baada ya kuungwa mkono na chama Fulani,au ni waziri,au kama mwanajeshi.''
Hakuna njia nyingje ile. Wabunge hao wanasema kuwa katiba haikubali mbunge yeyote kubadili chama bungeni.Ikiwa mtu atapoteza uungwaji mkono wa chama chake hii ina maana kuwa amepoteza kiti chake.
Lakini hilo limepingwa na mbunge muathiriwa na tena wakili, Wilfred Niwagaba.

Niwagaba alisema ''Ikiwa anadhani kwa kutusimamisha au kutufukuza uanachama ina maana kuwa tunapoteza viti vyetu,nasikitika sikubaliani na tafsiri hiyo.Hakuna hata mmoja wetu ameondoka kutoka chama kwa hiari.''

Hata hivyo mwenzao Vincent Kyamadidi amesimamishwa uanachama kwa muda kutokana na madai kuwa alilewa na kujaribu kupigana hadharani jambo ambalo linakwenda kinyume na maadili ya chama.
Aidha yeye alipoita kujieleza alifika mbele ya kamati hiyo.
Bado kuna vuta ni kuvute kuhusu majaliwa ya wabunge wanne, ikisemekana wamekwenda mahakani kupinga kufukuzwa kwao.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment