Tuesday, April 23, 2013

Soma maoni ya wadau wa jamii forum kuhusu mazoezi ya ndege za jeshi jijini Dar.


hivyo vindege hata manati yaweza kuvipopoa ..... tena wananchi wawe makini .... zaweza kulipuka zenyewe .... pale msata mwaka jana ndege vita imedondoka yenyewe.

hii ni sawa na kututisha.kwanini wasifanyie mapolini au baharini?hatutishwi na ndege.maandamano yapo palepale.

Hivyo vitisho tumesha zoea, bado mazoezi ya vifaru kwani mazoezi ya mabomu wamesha maliza, lakini atishiwi mtu nyani apa, vita mbele mpaka kieleweke. CCM mkifika 2015 kweli mnabahati

Wala Kikwete asitutishe na nyoka aliyekufa; midege yote ya kijeshi, vyombo vyote vya dola ni mali zetu sisi wenyewe ndio tunaozigharamia siku zote na wala hatukuviweka hapo kuwalinda mafisadi kwa namna yoyote ile!!!

Anaiga ya Gaddafi... anaweza tumia styre ie ile ya kubombardment kwa kutumia airfighter.

wasije wakayandondosha midege yenyewe mara ya mwisho kuwashwa ni miaka ya 80 wakati wa vita ya Amini, haiaminiki, wakafanyie huko anga ya baharini mbali na si kwenye anga ya makazi ya watu, tafadhali. 
Watu hatuna imani kabisa, juzi juzi tu wamefanya uzembe mabomu yamelipuka hatujasahau hata kidogo eti mazoezi ya ndege za kijeshi kwenye anga letu.

Wao ndiyo wanafanya sisi tusiwaamini.

kitendo hiki kwa sasa kinatutisha watanzania tulio wengi kwani hatuiamini tena serikali na vifaa vyake vya kijeshi. kama mkidondosha ndege au kugonga jengo this time no body will understand you kama gongo na mbagala things will change completely. kwanini msifanyie baharini bwana?????????

Jamani waacheni wafanye mazoezi kwani kinawauma nn?

Mwaka 1980 katika sherehe za mashujaa kulikuwa na parade kali ya kijeshi mbele ya Raisi Nyerere hapo uwanja wa Taifa huku ikisindikizwa na airshow; hiyo ilikuwa ndiyo sherehe ya kwanza ya mashujaa Tanzania baada ya vita ya Kagera. Kulikuwa na ndege ambazo nadhani zilikuwa tatu za kivita zikiwa zinavinjari anga lile na kuonyesha mbwembwe za angani. Kwa bahati mbaya mojawapo ilipata hitilafu na kuanguka mbele ya macho ya Nyerere karibu sana na kilipo Chuo Kikuu cha Elimu cha Chang'ombe na kumwua rubani wake; ni pembeni kidogo na ulipo uwanja wa Taifa mpya.

Baada ya ajali ile, Nyerere hakusema mengi katika hotuba aliyokuwa ameandaa badala yake aliwakumbusha wanachi kwa sentensi moja tu, kuwa mashujaa wetu walikumbana matukio mengi ya aina hiyo wakati wa kumwondoa nduli Amini. Kuna wengi waliopoteza maisha yao kama huyu shujaa tuliyeshududia maisha yake yakipotea mbele yetu. Sina kumbukumbu ya maneno kamili yaliyotumiwa na Nyerere kutoa ujumbe huo mfupi.


Nimekumbuka tukio lile kwa sababu wiki chache zilizopita kulikuwa na taarifa za wapiganaji wetu kuangua na ndege ya kivita huko Handeni na kupoteza maisha yao, na tukio la leo ambapo ndege ya kivita ilianguka huko Kanada na rubani akajirusha angani na kusalimisha maisha yake Ni kawaida kuwa kunapotokea hitilafu kwenye ndege za kivita huwa rubani anaiachia ndege ikajiangukie na yeye mwenye kuruka salama kwa mwavuli. Swali langu je sisi ndege zetu za kivita tulizinunua wapi zisiwe na mechanism ya kuokoa maisha ya rubani namna hiyo?

Kutoka: JAMII FORUM

No comments:

Post a Comment