Saturday, April 20, 2013

Suluhu ya Azam leo yawaweka pabaya kwa wamorroko.

 Naibu katibu mkuu wa CCM bara na mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba mwenye shati la kitenge, Rais wa TFF Leogdger Tenga (shati jeupe), kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelu 'julio' (fulana nyekundu) pamoja na wadau wengine wa soka wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko mechi ya leo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Wachezaji wa ASR Rabat wakicheza jaramba pembeni ya uwanja tayari kuenda kuongeza mashambulizi.

 Katibu wa TFF Angetile Osiah wa kwanza kulia akizungumza na kocha msaidizi wa ASR Rabat Lahcen Ouadani (wa kwanza kushoto) katikati ni kocha mkuu wa ASR Rabat Abderazzak Khair. Ilibidi katibu wa TFF aingilie kati kuwa mkalimani kwani makocha hao wanazungumza kifaransa hivyo ilikuwa tabu kidogo wakati wa mkutano na wanahabari baada ya mechi kuisha.


 Kocha wa ASR Rabat Abderazzak Kahir akimwambia kitu katibu wa TFF Osiah ili awaeleze wanahabari.


 Kocha msadizi wa Azam Kali Ongala akizungumza na wanahabari baada ya mchezo kuisha, kulia ni Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura.


Azam FC imeshindwa kuutumia vema uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Wamorocco AS FAR Rabat katika pambano la kwanza kuwania kuingia raundi ya tatu ya kombe la shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelsheli Azam walionekana kuchoka na kutumia muda mwingi kucheza pasi fupi katika kipindi cha kwanza. Hali kadhalika wapinzania wao wakawa wamejaza viungo wengi na mabeki ili kuhakikisha Azam hawapati bao hata moja.
Timu zote mbili zilipoingia kipindi cha pili zilicheza kwa kukamiana hasa Azam FC walimtumia mshambuliaji wao hatari Gaudience Mwaikimba aliyeingia kipindi cha pili kwa kupiga pasi ndefu na mashambulizi ya kushtukiza.

Lakini mpaka mwamuzi huyo kutoka visiwa vya shelisheli anamaliza pambano hilo si Azam si ASR Rabat aliyeona lango la mwenzie hivyo Azam kutoka macho chini kutokana na suluhu hiyo.

Na endapo Azam ingeshinda ingejiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele hatua ya makundi ya michuano hiyo migumu barani Afrika. Kwa sasa Azam watakuwa na kibarua kizito huko kaskazini mwa Afrika wiki mbili zijazo kwani watahitaji ushindi tu na si vinginevyo.

Akiongea baada ya mechi hiyo kocha msaidizi wa Azam, Kalimangonga Ongala alisema “Mechi ilikuwa ngumu lakini tulijitahidi kadiri ya uwezo wetu kupata walau goli moja, lakini suluhu si mbaya kwetu kwani inatuma mwanya wa kufanya mazoezi ya nguvu ili katika mechi ya marudiano tufanye maajabu.”

Kwa upande wake kocha wa ASR Rabat Abderazzak Khairi amesema lengo lao lilikuwa ni kushinda lakini hali ya hewa ya joto imewafanya wachezaji wake kuchea chini ya kiwango. Anategemea mechi ya marudiano watacheza vizuri katika uwanja wa nyumbani.

Aidha aliongeza Azam ni timu nzuri na amefurahishwa na viwango vya John Bocco na Gaudience Mwaikimba kwani walikuwa wakimnyima rah asana katika dakika za majeruhi.

HAFIDH KIDO
20 Aprili, 2013
Dar es Salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment