Tuesday, April 30, 2013

UINGEREZA KUACHA KUWAPA MSAADA AFRIKA KUSINI.



Uingereza imetangaza kuwa itakoma kutoa msaada kwa Afrika Kusini kuanzia mwaka 2015.


                     Waziri katika wizara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza Justine Greening


Waziri wa maendeleo ya kimataifa, Justine Greening, anatarajiwa kutangaza rasmi hatua hiyo itakayoinyima afrika kusini msaada wa moja kwa moja wa dola milioni thelathini kila mwaka baadaye hivi leo.
Maafisa wanasema hatua hiyo ni ya kutambua ustawi wa Afrika kusini tangu kukamilika kwa utawala wa kibaguzi, huku taifa hilo likionekana kuwa na uwezo wa kutoa msaada kwa mataifa mengine.
Katika hatua kama hiyo Uingereza ilisitisha kutoa msaada kwa taifa la India mwaka uliopita.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment