Tuesday, April 30, 2013

Wanajeshi wa Nigeria watembelea Tanzania.




 Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda  (kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali  Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea  ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.


Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja  na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao  kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa  ziara ya mafunzo ya siku tano.


 Baadhi ya  wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakimsikiliza Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati walipomtembea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.


NA MAGRETH    KINABO
                                                                     
ELIMU ya uzalendo imesaidia  kuwafanya  vijana  wa Kitanzania kuipenda nchi yao , hali iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa leo na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na  Michezo,Seth Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa  watu 22,baadhi yao ni viongozi wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu wa mafunzo ya   kijeshi  kutoka  Nigeria.
Ujumbe huo umetembelea wizara hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya  Utamaduni wa Kitanzania, umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja   Generali, Ati  John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo ya program tunazowafundisha  vijana ili kuondoa  migogoro  katika nchi  yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda nchi yao.  Elimu hii imesaidia  kupunguza migogoro,alisema.” Katibu Mkuu huyo alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi  hao   lililouliza kuwa  kuna program  zipi zinazochangia kupunguza migogoro  hususan kwa vijana.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi ili waweze kubuni miradi mbalimbali kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo vijana wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli  mbalimbali  kuwawezesha kiuchumi.
Aidha Katibu Mkuu huyo akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema wizara  yake ndi yenye jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo katikawizara hiyo yenye sekta nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 Kamuhanda  alisema sekta ya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
 Aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini  na ndiyo iliyoleta umoja ,amani na mshikamano.
 Wakizungumzia kuhusu ziara hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi,  Ikema Francis walisema wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya kiutamaduni na kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.
 IDARA YA HABARI- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment