Tuesday, April 30, 2013

Wasomi Australia wataka Profesa kuvuliwa udaktari.


Wasomi nchini Australia wametaka mpasuaji wa kichina anayetuhumiwa kufanya biashara haramu ya viungo vya mwili kuvuliwa taji la mtaalamu alilopewa katika chuo kikuu cha cha Sydney.
Huang Jiefu, aliyesomea taaluma hiyo huko Sydney, hivi maajuzi aliongezewa muda taji hilo la kuwa Profesa kwa miaka mitatu inayokuja.
Lakini wasomi kutoka kitengo cha afya cha chuo kikuu hicho wamemtaja kuwa bingwakwa jitihada zake katika kuleta mageuzi kwenye taaluam hiyo.
Chuo kikuu cha Sydney ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyo na sifa kuu nchini Australia.Mnamo mwaka 2005 Huang Jiefu,alikuwa afisa mkuu wa kwanza wa afya aliyefichua mtindo wa China kutoa viuongo vya mwili kutoka kwa wafungwa.
Na anatazamwa na wengi kama aliyeleta mageuzi katika katika mfumo huo unaoshutumiwa kwa ukubwa.
Kwa waliopanga ombi la kutaka apokonywe taji alilopewa wanaona kwamba anahusika na mfumo huo usio na maadili na amehusika katika hilo kwa kufanya upasuaji wa kutoa ma kubadili viungo hivyo.
Wanadai kuwa yeye na maafisa wa serikali Beijing wametoa malipo ili kusitisha biashara hiyo haramu.
Kw amujibu wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu China huua wafungwa takriban 4000 kila mwaka kwa kutumia sindano yenye sumu ili kutoa viungo hivyo katika miili ya wafungwa hao.
BBC SWAAHILI

No comments:

Post a Comment