Wednesday, April 3, 2013

Ziara ya Waziri Samia Suluhu yaleta matumaini Zanzibar...


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akifafanua Jambo wakati alipotembelea Mradi wa mpunga kwa njia ya umwagiliaji kwenye Bonde la Mpunga la Jendele; kulia ni Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali Mussa. 


 Mratibu wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za  Mpunga kwenye  Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipita kwenye shamba la mpunga la kuzalishia Mbegu la kinyasini-kisongoni Walaya ya Kaskazini A Unguja Waziri akiwa katika Ziara ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na ASSP [Picha na Ali Meja ]  


Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan amesema  kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kuitunza na kuindeleza miradi inayofadhiliwa na Serikali zote mbili  na washirika wa maendeleo ili miradi hiyo indelee kuwanufaisha wananchi na kutimia lengo lililo kusudiwa.

Hayo ameyasema jana huko Jendele Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipofanya ziara  kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo iliyofadhiliwa na TASAF kupitia Serikali ya muungano Tanzania.

Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi kufadhili wananchi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa lengo la kuwaweze kujikwamua na umasikini ili kujipatia kipato.

Amesema wananchi wajifunze kuitunza na kuendeleza miradi hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufaisha wenyewe.

“kuiacha miradi ife si vizuri, muichangie ili iweze kujiendesha na hiyo ndiyo faida ya miradi hiyo”, alisema Samia.

Aidha Waziri aliwaambia wakulima wa bonde la Jendele Kinyasini Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa hakuna sababu kwa vile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo hivyo  uzalishaji ungezeke.

Waziri huyo alisema dhamira ya ziara yake kuja Zanzibar ni kuona vipi matumizi ya pesa za TASAF zinavyotumika katika miradi iliyoombewa na utekelezaji wake umefikiaje kwa wananchi.

Waziri alifurahishwa na juhudi zinazochukuliwa kwani kumefikiwa hatua kubwa za kimaendeleo na zinatia matumaini.

Waziri alitembelea mradi wa  mpunga na mradi wa uzalishaji mbegu za mpunga Kinyasini kisongoni na badaye kupata maelezo juu ya miradi ASSP na SPDL inayoendeshwa na Wizara ya Kilimo, Maliasili na Ushirika Zanzibar .

Miradi yaTASAF awamu ya kwaza Zanzibar   ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu ambapo ziligawanywa  sawa kwa Unguja na Pemba.

Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani 2,500.000.00  ambapo zilitumika kumalizia mradi wa kwaza Unguja na Pemba kupitia mifuko mitatu nayo ni mfuko wa Taifa wa kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs 2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya fedha TShs 1,800,000.000.00.

Ziara hiyo itaendelea leo kutembelea idara ya uhamiaji Zanzibar na malaka ya kitambulisha cha Taifa Zanzibar.

HAFIDH KIDO
4 April, 2013  




No comments:

Post a Comment