Thursday, May 16, 2013

Beckham atangaza kustaaf soka...

Nahodha wazamani wa timu ya Soka ya Uingereza David Beckham ameamua kustaafu mwisho wa msimu huu.

Beckham mwenye umri wa miaka 38 alijiunga na timu ya Paris St-Germain mapema mwezi wa Januari kwa kandarasi ya miezi mitano.

Wakati wa kutia saini kandarasi hiyo mwamba huyo wa Uingereza alitangaza kwamba mshahara wake wote atautoa kwa mashirika ya kutoa msaada.

Beckham alijunga na timu ya Manchester United akiwa na umri wa miaka 14 na kufaulu kuichezea klabu hiyo mara 398 huku akishinda makumbe sita ya Ligi kuu na kombe la klabu bingwa bara Ulaya.

"Naishukuru sana timu ya PSG kwa kunipa fursa ya kuendelea kucheza lakini nahisi kuwa huu ni wakati mzuri kwangu kumaliza kazi yangu ya kucheza mpira " amesema.

Pamoja na PSG kubeba kombe la Ligue 1 la Ufaransa , katika uchezaji wake Beckham amezoa jumla makombe 19 - 10 kati yao yakiwa ni makombe ya ligi kuu mbali mbali.

Bechkam ndie mchezaji wa kwanza wa Uingereza kuwahi kubeba makombe ya ubingwa wa Ulaya akichezea timu katika nchi nne tofauti.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment