Tuesday, May 7, 2013

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) Kampasi ya Dar es Salaam imesimamishwa kutoa shahada za uzamili (Masters) na uzamivu (PHD) na tume ya vyuo vikuu vya Tanzania (TCU).


Kampala International University, Dar es Salaam Constituent College (KIU-DCC)
KUSIMAMISHWA KWA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU
Kampala International University, Kampasiya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati naTumeyaVyuoVikuuTanzania (TCU).
Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasiya Dar-es-Salaam ifuatayo;
  1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam
  2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika program zilizotajwa hapo juu wawezekuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. 
Angalizo:
Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YAVYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

No comments:

Post a Comment