Sunday, May 12, 2013

Mshindi wa kwanza ligi ya soka Vodacom Tanzania bara kuchukua kitita cha Mil 70.

Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania Salum Mwalimu (katikati) akizungumza na wanahabari juu ya tuzo za mshindi wa kwanza wa ligi kuu ya soka Vodacom Tanzania bara, kushoto ni Ofisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF na kulia ni ofisa uhusiano wa umma Vodacom Matina Nkurlu, ambapo vodacom imetangaza kutumia milioni 200 kwa zawadi za washindi kwa ujumla.


Mdhamini wa Ligi Kuu ya soka Tanzana Bara, Kampuni ya Vodacom imetangaza kutumia kiasi cha Shilingi Mil 200 kwa ajili ya kutoa zawadi ya fedha taslimu katika ligi inayomalizika mei 18 ambapo sasa Machampioni wa msimu huu watajinyakulia Shilingi Milioni 70.
Mbali ya bingwa, Vodacom pia itatoa fedha kwa timu inayomaliza nafasi ya pili, ya tatu na ya nne katika msimamo wa ligi ambazo ni Sh. 35 Milioni, huku Sh. 25 Milioni na Sh. 20 Milioni zote zikiwa na ongezeko ikilinganishwa na zawadi za fedha zilizotolewa katika msimu wa 2012 / 2013.

Zawadi hizo zimetangazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kampuni hiyo kupitia Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim, ikiwa ni pamoja na kuainisha zawadi za washindi wa mchezaji mmoja mmoja pamoja na timu iliyoonyesha nidhamu kwa msimu huu.
"Mwaka huu tutatumia kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya zawadi za fedha taslimu kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom huku bingwa akinyakua kitita cha Shilingi Milioni 70 ikilinganishwa na Sh 50 Milioni za msimu uliopita." Alisema Mwalim.
Mwalimu amesema lengo la kuongeza zawadi ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wadhamini wa ligi na wadau wengine wa soka na kwa pamoja kuwa na dhamira ya dhati katika kuendeleza soka nchini.
"Kila mmoja ni shahidi wa namna ambavyo soka letu limekuwa na namana ambavyo tunakabaliana hatua kwa hatua na changamoto zinazohusiana na ligi. Ni matumaini yetu kwamba tunapiga hatua na tuna matumaini ya kufikia kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya soka nchini yanaonekana." Aliongeza Mwalim "Kwetu sisi kama wadhamini tutajitahidi kadri inavyowezekana kuhakiksha tunaleta mabadiliko katika soka la Tanzania, tunaangalia mpira wa miguu nchini kwa upana zaidi kama mchezo unaopendwa, unaotuleta pamoja kama taifa na kuitangaza nchi yetu. Falsafa yetu hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo utulivu na ushirikiano mzuri miongoni mwa wadau na hivyo kutuletea mafanikio." Alisema Mwalim Zawadi nyingine zilizo tangazwa ni pamoja na zawadi ya mchezaji bora wa Mwaka golikipa bora, na mfugaji bora kila mmoja anajinyakulia Shilingi Milioni 5.
Aidha, mwamumzi bora na kocha bora kila mmoja atajipatia Shilingi 7,500,000 kila huku timu iliyoongoza kwa nidhamu itapata zawadi ya fedha taslimu ya Shilingi Milioni 15.
"Tumekuwa na msimu mzuri uliojaa ushindani na hamasa, tunatarajia timu zitajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao na hivyo kuendelea kuipa ubora ligi yetu."Alisema Mwalim huku akiwashukuru wadau wa mpira wa miguu nchini ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, Chama cha Waamuzi(FRAT), Vilabu, wachezaji na kipekee washabiki na kamati ya ligi kuu.
Amesema bila ya ushirikiano wa wadau hao na wengine ikiwemo Serikali, ligi kuu ya Vodacom isingeweza kufikia maendeleo iliyoyafikia katika msimu unaomalizika ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na mpira wa uwanjani na si vinginevyo.
CHANZO: MATINA NKURLU

No comments:

Post a Comment