Tuesday, July 2, 2013

Habari picha ziara ya Tanga.

 Vijana wengi wa Mkoa wa Tanga kwa sasa wameamka na wanafanya kazi kwa bidii, ila ikifika jioni lazima wake maskani kujadili mambo yao. Kinachonifurahisha zaidi ni aina yao ya uvaaji, kofia.

Tanga bado wanashikilia utamaduni wa kutembeza bidhaa barabarani. Hasa msimu wa matunda ukianza hutembezwa barabarani kwa tumia baskeli kama wanavyochuuza samaki.
Wasichana vigoli zamani ilikuwa mwiko kukaa barazani, lakini sasa mambo yamebadilika.
Tanga mtu haoni tabu kufuga mbuzi hata mmoja. Anaona raha tu vile akienda malishoni na kurudi jioni.
Minazi ni mali inayoheshimika sana Mkoani Tanga.
Hii ni shule ya Sekondari Tanga Technical School, ndiyo shule aliyosoma Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Kazi ni kazi bora mkono uende kinywani.
Pweza ni samaki anayependwa sana mkoani Tanga.

Nilifika Tanga kukiwa na sherehe za Tamta Day, hivyo wasichana na kinamama walikuwa wamejipanga barabarani kuwalaki waalimu wa chuo hicho cha dini.

KIDOJEMBE

No comments:

Post a Comment