Monday, July 22, 2013

Jacob Zuma amwambia balozi wake Zimbabwe asijibizane na Rais Mugabe.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemtaka balozi wake nchini Zimbabwe kukoma kutoa matamshi hadharani baada ya kukosolewa na rais Robert Mugabe.
Zuma, aliyekuwa mpatanishi mkuu katika mgogoro wa kisiasa mwaka 2008-2009 nchini Zimbabwe, alisema ni yeye pekee anayeruhusiwa kutoa matamshi yoyote kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Julai tarehe 31.
Balozi wake Lindiwe Zulu, wiki jana alisema kuwa maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe hayaonekani kuridhisha.
Rais wa Zimbabwe ndiye alimtaka Zuma kumkomesha balozi wake dhidi ya kutoa matamshi kama hayo hadharani.
Rais Mugabe ananuia kuendelea kuongoza nchi hiyo hata baada ya kuitawala kwa miaka 33 na atamenyana na waziri mkuu wake Morgan Tsvangirai.
Mahasimu hao wa jadi wamekuwa wakigawana mamlaka tangu mwaka 2009, chini ya mkataba ulioafikiwa kwa usaidizi wa rais Zuma.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment