Friday, July 19, 2013

Mashahidi wawili dhidi ya Kenyatta ICC wajitoa kuhofia usalama wao.


Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda, amesema kuwa mashahidi wawili wametupilia mbali ushahidi wao katika kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Bi Bensouda alisema mashahidi nambari 5 na 426 wamefutilia mbali ushahidi wao kwa sababu za waswasi kuhusu usalama wao.
"kwa kifupi, inaonekana kuwa wasiwasi wa shahidi nambari tano, wameogopa sana kuhusu usalama wao na kuwa athari za kutoa ushahidi wake huenda zikawa na madhara makubwa kwa maisha yake na kwa hivyo akaamua kufutia mbali ushahidi wake.'' alisema Bensouda kwa ujumbe wake kwa majaji mnamo Jumanne.
Aliongeza kuwa upande wa mashtaka, ulikuwa umefanya mashauriano na shahidi nambari 426 kumtaka abadili msimamo wake, lakini mazungmzo hayakufua dafu.
"upande wa mashtaka umefanya mazungumzo na shahidi 426 kujua ikiwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa kuodnoa wasiwasi wake pamoja na kumwezesha kuhudhuria kesi. Mazungumzo hayo, hata hivyo hayakufua dafu baada ya kusisitiza kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi wake, '' aliongeza kusema Bi Bensouda said.
Hata hivyo mwendesha mashtaka aliwaaambia majaji kuwa ushahidi wao sio muhimu tena kwa ushahidi wake dhidi ya mtuhumiwa.
Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta itaanza kusikilizwa Novemba 12.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment