Tuesday, July 2, 2013

Obama aweka shada la maua kukumbuka wahanga wa bomu ubalozi wa Marekani mwaka 1998.


Rais wa Marekani Barack Obama ameweka mauwa kwenye makaburi ya waathiriwa wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998, kama ishara ya kuwakumbuka.
Raia 11 wamarekani waliuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na kundi la kigaidi la al-Qaeda ambaklo lilifanyika wakati mmoja na shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya.
Obama aliuungana na rais mstaafu wa Marekani George W Bush kwa kumbukumbu hizo.
Rais Obama yuko katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya pili ya Afrika akiwa rais , ambapo alitembelea Senegal na Afrika Kusini.
Aidha Obama pia atamtembelea kituo cha kuzalishha umeme kinachomilikiwa na Marekani nchini humo, kufuatia tangazo lake mwishoni mwa wiki la mradi wa umeme utakaogharimu mabilioni ya dola.
Mradi huo wa miaka mitano, unatarajiwa kusaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara,kwa ushirikiano na mataifa ya kiafrika pamoja na sekta binafsi.
Akiwa nchini humo, Obama pia anatarajiwa kuzindua mpango unaonuia kusaidia nchi za Afrika Mashariki ikiwemo, Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda kushirikiana kibiashara.
Wakati huohuo, mkewe Obama, Michelle anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa wake za marais, unaoandaliwa na taasisi ya George W Bush huku ukiongozwa na mkewe Laura Bush.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment