Wednesday, July 10, 2013

Wajukuu wa Mandela wazika tofauti zao.


Wajukuu wawili wa kike wake Nelson Mandela wamekua wakijibu maswali kupitia Twitter kuhusu mzozo unaoghubika familia hio kuhusu kufukua maiti na kuzikwa tena.
Zaziwe Dlamini-Manaway na Swati Dlamini wamesema Babu yao yuko shwari na kwamba familia imeungana pamoja. Wawili hao wamekua washiriki wakuu katika makala ya runinga "Being Mandela" na ambayo hupeperushwa nchini Marekani. Mzee Mandela amelazwa hospitalini akiwa na matatizo ya kupumua.
Taarifa ya afisi ya Rais Afrika Kusini imeendelea kusema kwamba hali ya Afya ya Mandela ni shwari. Kiongozi huyo wa zamani Afrika Kusini alifungwa jela miaka 27 kwa kupinga ubaguzi wa rangi. Aliachiwa huru mwaka wa 1990 na kuchaguliwa Rais mwaka 1994.
Aliachia madaraka baada ya kuhudumu kwa muhula mmoja.Katika siku za karibuni familia ya Mandela imekumbwa na mzozo dhidi ya eneo la kuwazika wanawe Mandela waliokufa miaka iliyopita.Mahakama iliamrisha maiti tatu za watoto hao kufukuliwa kutoka eneo la Mvezo na kurejeshwa eneo alikozaliwa Mandela la Qunu.
Kesi hio iliwasilishwa na jamaa wa Mandela waliomlaumu mjukuu wake Mandla Mandela kwa kufukua maiti bila kupata idhini ya familia na wazee wa kijamii na kisha kuzipeleka eneo la Mvezo kama njama za kuhakikisha Mzee Mandela anazikwa eneo hilo.
Bi Dlamini-Manaway na Ms Dlamini wamesema hawajafurahia tukio hilo lakini wakasema familia imeungana. Pia wamesema wanamheshimu binamu yao Mandla.Mabinti hao ni wanawe mwanawe Mandela Zenani Mandela, na Bibi yao ni aliyekua mkewe Mandela Winnie Madikizela-Mandela.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment