Friday, December 6, 2013

HOTUBA YA HUZUNI YA JACOB ZUMA KUIFAHAMISHA DUNIA KIFO CHA MANDELA




Ndugu zangu wana Afrika Kusini
Kipenzi chetu Nelson Rolihlahla Mandela,Rais wa kwanza wa taifa letu la kidemokrasia ametutoka.Ameaga dunia katika hali ya utulivu akiwa amezungukwa na familia yake,majira ya saa 2.50 usiku (saa 3.50 usiku Tanzaniai) leo tarehe 5 Disemba 2013.Na sasa anapumzika.Yupo kwenye amani.Taifa limepoteza mtoto wake kipenzi.Watu wetu wamepoteza baba.Ingawaje tulijua siku hii itafika,hakuna kitu kinachoweza kutupunguzia huzuni kuu ya kumpoteza.Mapambano yake yasiyokoma kupigania uhuru yamemletea heshima ulimwenguni.Tabia yake ya kutojikweza,upendo na utu aliokuwa nao,vilimfanya apendwe na watu.Mawazo na sala zetu tunaziweka kwa familia ya Mandela.Kwao tuna deni la shukrani.Wamejitolea na kukumbana na mambo mengi magumu ili watu wetu wawe huru
Mawazo yetu yapo kwa mkewe Graca Machel na mkewe wa zamani Winnie Madikizela-Mandela,watoto wake,wajukuu zake vitukuu vyake na ukoo mzima wa Mandela.Mawazo yetu yako pamoja na marafiki zake ,makomredi wenzake na wale aliokuwa nao bega kwa bega na Madiba kwenye maisha yake ya mapambano.
Mawazo yetu yako pamoja na watu wote wa Afrika Kusini,ambao leo wanalia kumpoteza mtu ambae, kuliko yoyote yule, aliweza kuunganisha fikra zao na kuunda taifa moja la kawaida.Mawazo yetu yako pamoja na mamilioni ya watu ulimwenguni
ambao walichukulia Madiba kama mtu wao na ambao pia walifanya harakati zake kama zao.
Huu ni wakati wa huzuni kubwa kwetu,taifa limepoteza mtoto wake kipenzi.

Tena kile kilichompa Mandela heshima kubwa ni kile kile kilichomfanya oenekane mwanadamu.Kwake tuliona vile tulivyokuwa tunatafuta.Na kwake tuliona mengi yanayotuhusu sisi wenyewe.

Ndugu zangu wa Afrika Kusini,Nelson Mandela ndie mtu alietuunganisha,na kwa muungano huo tutamuaga tukiwa pamoja.

Mpendwa wetu Nelson Mandela atapewa heshima zote za mazishi ya kitaifa.Nimeshaagiza bendera zote za Jamhuri ya Afrika Kusini zishushwe nusu mlingoti kuanzia tarehe 6 Disemba na ziendelee kuwa hivyo hadi shughuli za msiba zitakapofika tamati.

Wakati tunajikusanya kutoa heshima zetu za mwisho,tufanye mambo kwa utu na heshima ambazo Madiba alizibeba kwenye nafsi.Tukumbuke na kuheshimu vile alivyopenda vifanywe na vile ambavyo familia yake vinataka vifanyike.

Tunapokusanyika kuomboleza popote ndani ya nchi hii na popote pale duniani,tujikumbushe thamani ya mapambano ambayo Madiba aliyaendesha.Tukamilishe matarajio yake ya kuona jamii ambayo hakuna mtu anaenyonywa,kukandamizwa wala kunyang`anywa na mtu mwingine.

Tujitume katika mapambano ya pamoja-bila kubakisha nguvu na ujasiri tulivyo navyo-ili kujenga Afrika Kusini iliyoungana,isiyo ya ubaguzi wa rangi,ubaguzi wa kijinsia,ya kidemokrasia na yenye ustawi.Tujieleze ,kila mmoja kwa njia yake mwenyewe,katika kutoa shukrani za dhati kwa maisha ya mtu aliyoyatumia kuwatumikia watu wa nchi hii na katika harakati za kusaidia kuwainua wanadamu.

Kwa hakika huu ni wakati wa huzuni kuu kwetu,lakini pia uwe ni wakati wa kujenga nia kuu.

Nia ya kuishi maisha kama aliyoishi Madiba, kupambana kama Madiba alivyopambana na kutopumzika hadi pale tutakapotambua matarajio yake ya kuona Afrika Kusini iliyoungana kiukweli,kuona Afrika yenye amani na iliyostawi na kuona dunia iliyo bora.
Tutaendelea kukupenda siku zote Madiba!

NKOSI SIKELE`I AFRIKA (MUNGU IBARIKI AFRIKA)



English version.....
Nelson Mandela.
My Fellow South Africans,
Our beloved Nelson Rolihlahla Mandela, the founding President of our democratic nation has departed.
He passed on peacefully in the company of his family around 20h50 on the 5th of December 2013.
He is now resting. He is now at peace.
Our nation has lost its greatest son. Our people have lost a father.
Although we knew that this day would come, nothing can diminish our sense of a profound and enduring loss.
His tireless struggle for freedom earned him the respect of the world.
His humility, his compassion, and his humanity earned him their love. Our thoughts and prayers are with the Mandela family. To them we owe a debt of gratitude.
They have sacrificed much and endured much so that our people could be free.
Our thoughts are with his wife Mrs Graca Machel, his former wife Ms Winnie Madikizela-Mandela, with his children, his grand-children, his great grand-children and the entire family.
Our thoughts are with his friends, comrades and colleagues who fought alongside Madiba over the course of a lifetime of struggle.
Our thoughts are with the South African people who today mourn the loss of the one person who, more than any other, came to embody their sense of a common nationhood.
Our thoughts are with the millions of people across the world who embraced Madiba as their own, and who saw his cause as their cause.
This is the moment of our deepest sorrow.
Our nation has lost its greatest son.
Yet, what made Nelson Mandela great was precisely what made him human. We saw in him what we seek in ourselves.
And in him we saw so much of ourselves.
Fellow South Africans,
Nelson Mandela brought us together, and it is together that we will bid him farewell.
Our beloved Madiba will be accorded a State Funeral.
I have ordered that all flags of the Republic of South Africa be lowered to half-mast from tomorrow, 6 December, and to remain at half-mast until after the funeral.
As we gather to pay our last respects, let us conduct ourselves with the dignity and respect that Madiba personified.
Let us be mindful of his wishes and the wishes of his family.
As we gather, wherever we are in the country and wherever we are in the world, let us recall the values for which Madiba fought.
Let us reaffirm his vision of a society in which none is exploited, oppressed or dispossessed by another.
Let us commit ourselves to strive together - sparing neither strength nor courage - to build a united, non-racial, non-sexist, democratic and prosperous South Africa.
Let us express, each in our own way, the deep gratitude we feel for a life spent in service of the people of this country and in the cause of humanity.
This is indeed the moment of our deepest sorrow.
Yet it must also be the moment of our greatest determination.
A determination to live as Madiba has lived, to strive as Madiba has strived and to not rest until we have realised his vision of a truly united South Africa, a peaceful and prosperous Africa, and a better world.
We will always love you Madiba!
May your soul rest in peace.
God Bless Africa.
Nkosi Sikelel' iAfrika.


No comments:

Post a Comment