Saturday, December 28, 2013

Ingia ndani uone gari alilotumia Baba wa Taifa kuenda Airport kwa mara ya mwisho kabla ya kifo chake Uingrereza.Gari hili

Gari hili Maarcedes Benz (E300), lilitengenezwa Ujerumani Desemba 17, 1996. Aliletewa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Mara ya mwisho kulitumia ilikuwa ni Agosti 31, 1999 lilipompeleka Uwanja wa ndege akielekea Uingereza kuangalia afya. Lakini hakulitumia tena maana alifariki dunia miezi miwili baadae Oktoba 14, 1999. Mke wa Nyeye mama maria alilikabidhi kwa wakuu wa makumbusho ya taifa Septemba 24, 2004 kwa ajili ya kumbukumbu.
Gari hili Rolls Royce lilitengenezwa Uingereza Novemba 5, 1965. Aliletewa baba wa Taifa Mwalimu nyerere kwa matumizi ya kiofisi. Rais wa pili Ali Hassan Mwinyi alilitumia na rais wa tatu Benjamin Mkapa pia lilitumia kabla ya kupelekwa makumbusho ya taifa  Machi 2, 2006.
Gari hili lilitengenezwa nchini Uingereza mwaka 1938, likaja nchini mwaka huohuo kwa matumizi ya kiofisi kwa gavana Sir Harold MacMichael, gavana wa mwisho wa Tanganyika Sir Richard Turnbull pia alilitumia. Rais wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere alilitumia, lakini ilipofika mwaka 1978 alitaka liletwe makumbusho ya taifa. Lakini kabla ya hapo lilitumika kupokea wageni wa kitaifa. Miongoni mwa watu maarufu kulitumia ni Rais wa Liberia Marehemu William Tubman, na mfalme wa Ethiopia hayati Haille Selassie.
Gari hili Austin Morris (A40), lilikuwa likitumiwa na Mwalimu Nyerere katika harakati za Tanu. Liliendeshwa na dereva maalum Mzee Said Tanu. Baada ya kupata uhuru Mwalimu alilikabidhi kwa vijana wa Tanu kwa kazi za kichama.
Huu ndiwo ulikuwa mtambo wa zamani wa kuuza mafuta ya taa katika kituo cha mafuta cha British Petrolium (BP).

1 comment:

  1. Kwa hakika blog yako, imekaa kitaaluma mno...naitopfatisha na kuiweka mbali tena juu kabisa zaidi ya zile ambazo kila kukicha zinalipuka kwa pamoja na habari za utupu,mambo yasiyo ya kimaadili na habari zisizo leta siha ya ufahamu kwenye bongo zetu..BIG UPU kaka ongeza juhudi..endelea kupekuapekua yaliyojificha na sisi tufaidike.

    ReplyDelete