Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ,
inakamilisha maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika
tarehe 26 Agosti, 2012. Ili kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi
za kazi za muda za MAKARANI NA MAKARANI WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania
wenye nia na sifa zinazostahili kama
ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na
kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.
1. KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii,
endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na
atakuwa na kazi zifuatazo:-
a) Kuhudhuria mafunzo ya
kuhesabu watu;
b) Kuhesabu watu kwa
kutumia dodoso fupi katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu
anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c) Kutunza vifaa vyote
na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d) Kufanya kazi nyingine
zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii
anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi
miaka 60 na mwenye afya njema;
b) Awe amehitimu angalau
kidato cha nne;
c) Awe ni Mkaguzi au
Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule
ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi
yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu
masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote
ya jinai.
2. KARANI MWANDAMIZI WA
SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii,
endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na
atakuwa na kazi zifuatazo:- 2
a) Kuhudhuria mafunzo ya
kuhesabu watu,
b) Kuhesabu watu kwa
kutumia dodoso refu katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu
anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c) Kutunza vifaa vyote
na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d) Kufanya kazi nyingine
zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii
anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi
miaka 60 na mwenye afya njema,
b) Awe amehitimu angalau
kidato cha sita,
c) Awe ni Mkaguzi au
Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule
ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi
yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu
masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote
ya jinai.
3. Namna ya Kutuma
Maombi
Mtanzania mwenye sifa
zilizotajwa hapo juu atume maombi yake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya
Wilaya/Halmashauri kwa anuani iliyowekwa hapa chini, akiambatisha nakala za
vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa alizonazo.
Maombi hayo yatumwe kwa
kujaza Fomu Maalum ya maombi ya kazi ambayo inapatikana katika Ofisi ya Mratibu
wa Sensa wa Wilaya/Halmashauri, na endapo fomu haikupatikana, mwombaji atume
maombi kwa kuandika barua akionyesha anuani kamili ya mahali anapofanyia kazi
na namba ya simu kama anayo.
Maombi yapitishwe kwa
wakuu wa kazi kwa walioajiriwa au Watendaji wa Mtaa/Kijiji kwa wale wasiokuwa
na ajira, ili maombi hayo yafike wilayani kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Sensa ya Wilaya
Wilaya ya ………………………..
S.L.P……………………………….……
Bofya maandishi
yafuatayo kupakua:
Fomu
ya KUKUBALI Kazi - SENSA
No comments:
Post a Comment