Taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya
Marekani itaipatia Kenya ndege nane ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu
ya msaada wa kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na
wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab.
Gazeti la Wall
Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege hizo ambazo
hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa kulengwa na
ndege au majeshi ya ardhini.
Gazeti
hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni
sehemu ya msaada wa Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha
kwa Burundi , Djibouti na Uganda .
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:
Post a Comment