Kiongozi wa wanajeshi walioasi nchini Madagascar amepigwa risasi na
kuuwawa kufuatia makabiliaono makali na wanajeshi watiifu.
Awali jeshi lilikomboa kambi ya kijeshi iliyokuwa ikimilikiwa
na wanajeshi waasi baada ya makabiliaono makali.
Kulishuhudiwa ufyatulianaji wa risasi siku ya
Jumapili katika kambi ya kijeshi iliyokaribu na uwanja wa ndege wa Antananarivo ,ambapo
maafisa wa serikali wanasema watu watatu waliuwawa.
Katika
muda wote wa mapigano safari zote za ndege zilihairishwa.
Makao
makuu ya jesji ilithibitisha kwamba siku ya Jumapili kulitokea maasi yaliongozwa
na wanajeshi kadhaa.
Mashahidi
walisema kwa walishuhudia makabiliano ya risasi kwa zaidi ya saa nne nzima
ambapo watu walikusanyika kuangalia makabiliaono hayo.
Polisi
na wanajeshi walizingira eneo hilo
na kuhamisha watu kutoka baadhi ya majengo.
Maafisa
wakuu walitumwa kwenda kufanya mazungumza na wanajeshi waasi lakini taarifa
zinasema kuwa mmoja ya maafisa hao alipigwa risasi na kuuwawa.
Jeshi
linasema baada ya mazungumzo kugonga mwamba iliwabidi waanzishe harakati za
kukomba kambi hiyo kutoka kwa waasi.
Na
katika makabiliaono yaliofuatia ,kiongozi wa waasi na mwanajeshi mwengine
waliuwawa.
Sababu
za maasi hayo hayajatolewa.
Lakini
jeshi la Madagascar
linahusika sana
katika saiasa za nchi hiyo kwani mwaka wa 2009 lilimmunga mkono kiongozi wa sasa
Rajoelina kuchuykua uongozi kutoka kwa Marc Ravalomanana.
Mwaka
wa 2002, jeshi vile vile lilimsaidia Bwana Ravalomanana tonyakua uongozi baada
ya kuongoza maandamano wa kupinga serikali ya ki-marxi iliyokuwepo.
kua
uongozi baada ya kuongoza maandamano wa kupinga serikali ya ki-marxi
iliyokuwepo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment