Bodi ya Wakurugenzi ya
Benki ya NBC imemsimamisha kazi kwa kumpa likizo Mkurugenzi Mtendaji wa benki
hiyo , Lawrence Mafuru kupisha uchunguzi wa kukiuka taratibu za utendaji ndani
ya taasisi hiyo maarufu ya fedha nchini.
Kwa mujibu wa Taarifa
iliyotolewa jana na benki hiyo na kutiwa saini na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki hiyo, Mussa Assad, uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia
malalamiko ya wafanya wa NBC yakimtuhumu Mkurugenzi huyo kuwa alikuwa anakiuka
taratibu za kiutendaji.
“Bodi ya Wakurugenzi wa
NBC imepokea malalamiko ya wafanyakazi kuhusu kuwapo ukiukwaji mkubwa wa
taratibu za kiutendaji katika uongozi wa benki.”
Alisema Assad katika
taarifa hiyo na kuongeza:
“NBC ni benki
inayoheshimika na kuaminika, kwa hiyo ili ya kulinda taratibu na misingi ya
utawala bora, imeanza kufanya uchunguzi wa kina na sahihi juu ya tuhuma hizo.
Naye mafuru kwa up-ande
wake alisema; “ Nitatoa ushirikiano kwa dhati kuhakikisha kuwa uchunguzi juu ya
tuhuma zinazonikabili unafanyika kwa uhuru na haki.”

No comments:
Post a Comment