Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson
akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa
katika Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania katika Umoja wa
Mataifa. Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na
tukio la ajali ya kuzama kwa meli na hasara iliyotokana na
ajali hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni
miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na
kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa
katika Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa
Hii hapa taarifa kamili...
Na: Mwandishi Maalum
Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa,Mhe. Jan Eliasson ametoa salamu za pole kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufutia ajali ya kuzama kwa meli iliyotokea
hivi karibuni.
Katika salamu zake
ambazo amezitoa wakati akisaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika
Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Naibu Katibu Mkuu
amesema, ameshtushwa na kuguswa sana na taarifa za tukio la kupinduka na
hatimaye kuzama kwa meli, tukio ambalo limesababisha kupotea kwa maisha ya
watu.
“ Ninapenda kutoa salamu
zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wa
pande zote mbili. Nimeguswa sana
na taarifa hizi, sala na dua zangu zinakwenda kwa wahanga wote wa tukio hili.
Mimi Binafsi na Umoja wa Mataifa tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ”
Amesema Naibu Katibu Mkuu.
Katika mazungumzo yake
na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu, Mhe. Jan Eliason
amesema anaifahamu vema Tanzania
na kwamba miaka miwili iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.
“ Ninaifahamu vizuri sana Tanzania ,
nimefanya kazi kwa karibu sana na Dkt. Salim
Ahmed Salim, bado ninakumbukumbu nzuri sana za Tanzania .
Na nililikuwa kisiwani Zanzibar kama miaka miwili hivi iliyopita. Kwa kweli tukio hili
limenigusa sana ”.
Akasema Naibu Katibu Mkuu raia wa Sweden ambaye aliteuliwa hivi
karibuni kushika nafasi iliyoachwa na Dkt. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika hapa
Ubalozini kutoka salamu zao za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwa Watanzania wote .
Chanzo: Mjengwa
No comments:
Post a Comment