Saturday, July 21, 2012
kamera yetu mtaani leo....
Leo ni siku ya jumamosi, watoto wanakuwa wengi mtaani. Saa tatu asubuhi hii watoto wanacheza mpira wa miguu, hawa ni kina Mrisho Ngassa wa baadae lakini hawaandaliwi mazingira. Hiki ni kiwanja cha mtu, je serikali viwanja vyenu viko wapi ili watoto hawa wapate sehemu za kucheza siku za jumamosi na jumapili? Chukulia kiwanja hiki mwenyewe akiamu kujenga, watoto hawa watacheza wapi? Tafakari, chukua hatua.....
Napenda sana utaratibu wa maisha ya mwafrika, kila siku asubuhi lazima afue nguo.
Jumamosi hii jamani, watoto wanazagaa tu mitaani hawana viwanja vya kufanyia michezo. Wengi huishia kuenda kuokota vyama chakavu ili wapate vijisenti vya kununulia ubuyu, matokeo yake wakinogewa na pesa hawaokoti tena vyuma bali wanishia kuwa wezi...
Mtaani kwetu ukibeba monitor watu wanjua ni video (TV)...
Huyu dada hajauona mwezi leo, umeona kikombe cha uji pembeni kuleee..
Hili ni daraja lamto wa ng'ombe eneo la Tandale shule, watu wamekatazwa kutupa takandani ya mtaro, lakini wabishi sana kuelewa. Matokeo yake watoto wao na wao wenyewe hupata maradhi ya mlipuko...
Hiki ni kijiwe cha kahawa katika kituo cha Tandale Shule, lakini leo nilitegemea kitafungwa kwasababu ya mwezi wa mfungo. lakini jamaa kumbe hawajauona mwezi...









No comments:
Post a Comment